THE big boss wa The Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu
ametundika mtandaoni picha zinazoonesha mapaja yake jinsi
yalivyoharibika na kuweka michirizi ambapo alipoulizwa na shushushu wetu
kulikoni, alisema kuwa hataacha mkorogo hadi maduka yafungwe.

..Mapaja ya mrembo huyo.
Baadhi ya marafiki zake walianza kujadili namna alivyoharibika na
wengine kudai matumizi ya vipodozi vikali maarufu kwa jina la mkorogo
ndiyo vimemfanya apasuke kiasi hicho.Wema, baada ya kupokea maoni mengi juu ya picha hizo mengine yakiwa ni ya kejeli, aliwajibu kwa kuandika kuwa hataacha matumizi ya mkorogo hadi maduka yanayouza yafungwe.
Wema alipotafutwa na gazeti hili ili aweze kuweka wazi madai haya hakutoa ushirikiano kufuatia simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.
Source:Global Publisher

0 comments:
Post a Comment