WAZIRI Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye juzi aligeuka mbogo, baada ya
kukubaliana kwa kauli moja na wakazi wa Kijiji cha Kiluvya A, kuwatimua
maofisa wa Idara ya Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, ambao
walikwenda kuwashawishi wananchi wakubali kugawa ardhi yao bila
kuwashirikisha. Sumaye alikuwa mmoja wa wakazi wa kijiji hicho,
waliohudhuria mkutano uliyofanyika ofisi za Serikali ya mtaa ya kijiji
hicho.
Sumaye alikuja juu, baada ya Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa
Kisarawe, Constantine Mnemele kueleza sababu za ujio wao ndani ya kijiji
hicho.
Alisema wamefika kijijini hapo, ili kuwaeleza wananchi
namna ambavyo wanataka kugawa ardhi yao kwa ajili ya maendeleo ya mji wa
Kisarawe.
Jambo kubwa ambalo lilionekana kumsikitisha Sumaye na
wanakijiji wengine, ni pale Mnem
ele alipowaambia wanakijiji wawe tayari
kutoa ardhi yao kwa zaidi ya asilimia 40.
Kauli hiyo, ilionekana
wazi kuibua hasira za wanakijiji hao, ambao kwa kauli moja waliwataka
watendaji hao waondoke mara moja katika mkutano huo.
Mnemele,
alisema asilimia 15 ya eneo litakalochukuliwa ni kwa ajili ya
uhamasishaji na michoro na asilimia tano ni miundombinu ya barabara na
fidia asilimia 12 zitarudi halmashauri, huku asilimia nane itakwenda kwa
wazabuni.
SUMAYE NA KAULI
Baada ya maelezo hayo, Sumaye ambaye ni mkazi wa Kiluvya A, aliomba kupewa nafasi ya kuzungumza.
Alianza
kwa kuwarushia makombora watendaji hao kuwataka waondoke katika mkutano
huo ili wakajipange upya na kusema huo ni ujanja wa kutaka kuwapora
ardhi wanakijiji.
Alisema hakuna mtu anayekataa maendeleo katika
kijiji chao, lakini ujanja wanaotumia halmashauri hiyo, ni jambo ambalo
haliwezekani kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kuwadhulumu.
“Nilichokuwa
nategemea kukiona hapa, ni ninyi watendaji mngekuja na ramani ili
mtuonyeshe wanakijiji na kutuomba jinsi ya kushiriki taratibu zote za
mipango miji, tunashangaa kuona kila kitu mmejipangia wenyewe bila
kutushirikisha, jambo hilo ni gumu kwetu.
“Nimeishi katika kijiji
hiki miaka mingi, tena wakati huo kulikuwa pori kubwa hata barabara
hazikuwepo zaidi ya kung’atwa na mbung’o, eti leo mnakuja mnataka
asilimia 40 za wanakijiji zinatoka wapi? Alihoji Sumaye.
Baada ya
maelezo hayo, Sumaye na wanakijiji wenzake kwa kauli moja waliunga
mkono na kuvunja mkutano huo, ili kutoa fursa kwa watendaji wa
halmashauri hiyo warudi wajipange upya.
Naye Ofisa Ardhi wa
Wilaya ya Kisarawe, Alkard Machum aliwaambia wanakijiji hao kuwa
pendekezo la asilimia 40, lilikuja baada ya mkurugenzi wa halmashauri
hiyo kukosa fedha za kuwalipa fidia wananchi. CHANZO MTANZANIA.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / WAZIRI MKUU MSTAAFU AWAFUTA KAZI MAAFISA IDARA YA ARDHI WILAYA YA KISARAWE MKOANI PWANI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment