Mshambuliaji wa timu ya soka ya Moro Sisters, Khadija Shabaan kulia akinyanyua daruga wakati akiwania mpira dhidi ya mlinzi wa Sega Sekondari, Subira Mohamed kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi ya soka ya wanawake Manispaa ya Morogoro yaliyoanza kutimua vumbi kwenye uwanja wa Moro Veteran ambapo katika mchezo huo Sega ilitandikwa bao 6-0 mkoani hapa.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
LIGI
ya soka ya wanawake Manispaa ya Morogoro imeanza kutimua vumbi huku
Moro Sisters ikitoa onyo kali kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo kwa
kuibuka na ushindi mnono wa bao 6-0 katika mchezo wake wa ufunguzi
uliofanyinyika kwenye uwanja wa Moro Veteran mkoani Morogoro.
Katika
michezo ya ufunguzi ilishihudia timu ya shule ya sekondari ya Uwanja wa
Taifa ikipokea kipigo cha bao 4-0 kutoka kwa Kihonda sekondari wakati
Sega sekon
dari nayo ikitandikwa bao 6-0 dhidi ya Moro Sisters.
Wafungaji
wa bao la kwanza katika kila mchezo wa michezo ya ufunguzi walizawadiwa
Tsh10,000 na Mwenyekiti wa Morogoro Press Club Idda Mushi ambao ni
Emiliana Amani wa timu ya Kihonda na Mwanaidi, Omari wa Moro Sisters.
Mshambuliaji,
Mwanaidi Omari aliiwezesha timu yake ya Moro Sisters baada ya kufunga
bao sita pekee yake kufuatia ushirikiano mzuri kutoka kwa Ummy Michael,
Monica Sadiki na Zena Ally waliotoa pasi za mwisho na kufunga bao hizo
dhidi ya Sega sekondari.
Katika
mchezo wa kwanza uliowakutanisha Uwanja wa Taifa dhidi ya Kihonda,
mshambuliaji, Elimiana Amani alifunga bao mbili wakati Lilian Temu
akipachika bao moja huku mlinda mlango wa Uwanja wa Taifa, Tumaini
Mwakibete aliizawadia wapinzani bao la nne wakati akiwa katika harakati
za kuokoa shuli lililoelekezwa langoni kwake na kufanya mchezo huo
kupoteza kwa bao 4-0.
Ligi
hiyo yenye lengo la kusaka wachezaji ambao wataunda timu ya soka ya
mkoa wa Morogoro imeanza julai 10 ikishirikisha timu tano za sekondari
ikiwemo Kizunga, Sua, Uwanja wa Taifa, Sega na timu ya Moro Sisters
ambapo ligi hiyo itahitimishwa julai 12 mwaka huu kwenye uwanja huo wa Moro Veterani.
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment