BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LORI LILILOBEBA MABOMBA YA KUSAFIRISHA GESI LASHAMBULIWA KWA MAWE HUKU DEREVA AKIDAIWA KUJERUHIWA MJINI MTWARA

HABARI zilizotufikia kutoka mjini Mtwara Zinasema kuwa Gari lililobeba Shehena ya Mabomba ya Kusafirishia gesi kutoka Mjini Mtwara kuelekea Dar limeshambuliwa na mawe na kupelekea dereva wa lori hilo Kujeruhiwa vibaya. 
Lori hilo lilianza kushambuliwa mara baada ya kuingia katika Manispaa ya Mikinda Mtwara Mjini sababu ya kushambulia gari hilo ni katika kile kinacho dhihir
isha kuwa wanamtwara bado hawajakubaliana na hoja ya Serikali ya kutaka kusafirisha gesi hiyo kwa ajili ya manufaa ya nchi. 

Lori hilo kwa sasa lipo kituo kikubwa cha polisi  Mtwara, ikiwa
ni wiki moja tu imepita tokeaa watu kadhaa kukamatwa na jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kile kinachodaiwa kusambaza waraka wa kuhujumu miundombinuu yote ya gesi mara tu serikali itakapo anza utekelezaji wake wa ujenzi wa bomba hilo kupeleka Dar.
Source: Jamii Forum
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: