TAASISI ya Haki za Binadamu nchini Syria imeeleza kuwa, zaidi ya
Misikiti 1,400 imebomolewa nchini humo tokea kuanza machafuko ya ndani
yapata miaka miwili iliyopita.
Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo ya
haki za binadamu nchini Syria inaeleza kuwa, tokea kuanza mashambulizi
ya magaidi mwaka 2011 kwenye maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, zaidi ya
misikiti 1450 na vituo kadhaa vya turathi za Kiisl
amu vimebomolewa
kabisa.
Taasisi hiyo imekosoa vikali uharibifu wa misikiti na vituo
hivyo vya kidini vya Waislamu nchini Syria na kusisitiza kuwa, uharibifu
huo hautawazuia kutekeleza ibada zao.
Makundi ya kigaidi ambayo
yanapata uungaji mkono wa kifedha, kisilaha na vyombo vya habari kutoka
baadhi ya nchi za eneo kama vile Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na zile
za kimataifa kama vile Marekani na Uingereza yameshadidisha mashambulizi
dhidi ya Syria, nchi ambayo ni mhimili wa muqawama dhidi ya utawala wa
Kizayuni wa Israel.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment