Christian
Mwakapusya Mtanzania anaeishi Marekani akiwa amembeba mtoto Joshua
Joseph baada ya kumtembelea nyumbani kwao Iyunga Jijini Mbeya.
David
Mwakapusya ambaye alifuatana na Baba yake akitoa msaada wa nguo kwa
mtoto ambaye hakufahamika jina lake kwa niaba ya watoto wanaoishi katika
mazingira magumu mtaani hapo.
Baadhi ya Majirani wa familia ya Joshua wakiwa na nguo walizopewa na Christian Mwakapusya
Christian Mwakapusya akizungumza na mama mlezi wa mtoto Joshua Joseph Nyumbani kwake Iyunga Jijini Mbeya.
Christian
Mwakapusya akizungumza na Amina Mwasankinga aliye simamishwa masomo kwa
kisingizio cha ushirikina alipo kutana naye katika Ofisi za Mbeya yetu.
MTANZANIA
anayeishi Marekani Christian Mwakapusya aliyeguswa na kitendo alichofanyiwa mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili kufungiwa
ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja
na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.
Kutokana na
kuguswa na tukio hilo Mtanzania huyo amelazimika kumtembelea Nyumbani
anakoishia na kujionea hali halisi aliyonayo mtoto huyo kwa sasa.
Akizungumza
kwa masikitiko nyumbani kwao eneo la Iyunga Mwakapusya amesema Wazazi
wanaofanya vitendo kama hivyo wanapaswa kulaaniwa na kukemewa.
Mwakapusya
aliyekuwa amefuatana na Mtoto wake wa Kiume David waliofunga safari kutoka
Marekani hadi Mbeya kumwona Mtoto huyo wametoa zawadi mbali mbali zikiwemo Nguo
na fedha taslimu alizokabidhiwa Mama mlezi pamoja na Balozi wa Nyumba kumi.
Mhanga wa
tukio hilo, Joshua Joseph umri unao kadiriwa kuwa ni kati ya miaka miwili
au mitatu ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake
wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao .
Balozi wa
mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza
kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na
maradhi ya utapiamlo.
Amesema
katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea taarifa kuhusiana
na suala hilo ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni
aliitwa katika ofisi za mtaakwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
Wakati huo
huo Msamaria mwema huyo kutoka Nchini Marekani pia amezungumza na Mwanafunzi
mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Amina Mwasankinga ambaye alifukuzwa Shule kwa
kisingizio cha Ushirikina.
Aidha amemuahidi
kumsaidia ili aweze kumaliza masomo yake huku akilaani vikali kitendo cha
Walimu wa Shule ya Hollwood ya Wilayani Mbozi kuamini imani za Kishirikina na
kumharibia masomo Mwanafunzi huyo.
0 comments:
Post a Comment