MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, imesema haina uwezo wa
kusikiliza kesi ya ugaidi inayowakabili makada watano wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Makada hao wanakabiliwa na shitaka la
ugaidi, ambapo Juni 24, mwaka huu, waliachiwa huru na Mahakama ya
Wilaya ya Igunga, kisha na wakakamatwa kwa tuhuma za kummwagia tindikali
kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Tesha, katika uchaguzi mdogo
wa Jimbo la Igunga, Mkoa wa Tabora, uliofanyika mwaka 2011.
Katika
kesi hiyo, watuhumiwa ni Evodius Justunian (30), mkazi wa Bukoba, Oscar
Kaijage, mkazi wa Shiny
anga, Seif Magesa wa jijini Mwanza na Rajabu
Daniel, mkazi wa Dodoma.
Watuhumiwa hao, walipokamatwa
walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga, kabla ya Katibu wa
Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo kukamatwa na kuunganishwa
kwenye kesi hiyo.
Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Tabora, Issa Magoli, alisema mahakama hiyo haina uwezo
kisheria wa kusikiliza shauri hilo ambapo aliliahirisha hadi Julai 22,
mwaka huu.
Kutokana na hali hiyo, Hakimu Magoli, aliwashauri
mawakili wa upande wa utetezi, kuwasilisha hoja zao Mahakama Kuu ya
Tanzania kwa kuwa huko ndiko kunakoweza kupatiwa ufumbuzi wa kisheria wa
shauri hilo.
Katika shauri hilo, washitakiwa hao walifunguliwa
kesi mbili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, baada ya kesi
ya awali ya kudhuru mwili kwa tindikali kufutwa na kufunguliwa kesi ya
ugaidi dhidi ya makada hao wa Chadema.
Awali, katika shauri hilo
yalizuka mabishano ya kisheria kati ya mawakili wa upande wa utetezi,
wakiongozwa na Peter Kibata na Profesa Safari, huku upande wa Serikali
ukiongozwa na Wakili Juma Masanja na Edifonce Mkandala.
Wakati wa
mabishano hayo, mawakili wa upande wa utetezi waliomba Mahakama ifute
kesi hiyo, kwa kile walichosema kuwa ni batili kutokana na baadhi ya
vifungu vya sheria kukiukwa, huku mahakama hiyo ikiwa haina uwezo wa
kuisikiliza isipokuwa Mahakama Kuu peke yake.
Mawakili hao
walisema kuwa, washitakiwa walikamatwa sehemu tofauti, hivyo kesi zao
zilipaswa kusikilizwa katika maeneo waliyokamatiwa badala ya kusikilizwa
katika eneo moja.
Ulinzi mahakamani.
Kabla ya washtakiwa
hao kufikishwa mahakamani, Jeshi la Polisi mkoa hapa liliimarisha ulinzi
katika eneo la mahakama ambapo ilipotimu saa 4 asubuhi, walifikishwa
wakiwa katika gari la Polisi lenye namba za usajili PT 1816, huku
wakiongozwa na askari wa kutuliza ghasia FFU. CHANZO MTANZANIA.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI TABORA HAINA UWEZO WA KUSIKILIZA KESI YA UGAIDI, YAWATEMA MAKADA WATANO WA CHADEMA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment