Akatoka Tabora mpaka Ujiji.Kufika Ujiji ipo
meli.Akaingia mpaka Kongo.Kufika Kongo moja kwa moja akaenda
akaukumbatia mlingoti wa bendera ya Ubelgiji.Akaulizwa haya nini shida
yako?.Akasema shida yangu mimi bwana nafukuzwa na Muiengereza,na sijui
akanipata kama ataniwacha hai au ataninyonga.
Akaambiwa
hapa hapana Muiengereza wala mdachi wala nani atakayeweza kukupata. Kaa
kitako.Baada ya kukaa kidogo ndipo alipopiga simu kwa jamaa zake
Tabora.
Swali:Ni mji gani wa Kongo alipokaa?.
Jibu:Ni
mji wa Kasongo,Kongo.Alipiga simu kwa Nassor bin Muhammed akawaambia
kwa haraka sana nileteeni mwanangu kwa sababu hali yangu ni dhariri
sasa.Kwa maana alipofika goti lilikuwa limevimba halifanzi kazi kutokana
na mwendo na dhiki iliyompata.Kweli nikachukuliwa nikapelekwa Kongo
nikamuwahi marehemu baba.
Swali:Katika Familia yenu mlikuwa muko wangapi?
Jibu:Kwa hapa Afrika alikuwa kanizaa mimi peke yangu.
Jibu:Kwa hapa Afrika alikuwa kanizaa mimi peke yangu.
Swali:Turudi Kongo.
Jibu:Nilipofika
Kongo tukaonana na marehemu baba lakini kwenda hawezi tena.Akasema jee
umefika mwanangu,akachukua kalamu na karatasi akaandika .
Kulikuwa na bwana mmoja wa Kisangani akiitwa Salim bin Amraan Al Maamry na mwengine akiitwa Nassor bin Salim AlHarmy ,alikuwa mtu mkubwa katika Kongo.
Akawaambia nawakab
idhi mwanangu huyu.Pindi nikiwa hai ninaye mwenyewe,lakini pindi Mwenyezi Mungu akinipa mauti basi asiwekwe pahala popote .Fanzeni hima apelekwe mpaka Unguja halafu apelekwe Oman.
Kweli haikuchukua muda mkubwa Mwenyezi Mungu akamukhitarisha,na mimi sikuwa na maisha ya kuketi pale tena.
Watu wakafanza utaratibu wakanipakia ndani ya meli mpaka Kigoma.Kufika Kigoma nikapakiwa ndani ya garimoshi mpaka Darisalama.
Kufika Darisalama nikaja mpaka Unguja nikakaa mwaka mmoja kwa baba yetu mdogo,sheikh Suleiman bin Said Alruweihy.
Swali:Ni eneo au mtaa gani huko Unguja?
Jibu : Ni Michungwa miwili.Baada ya muda huo baba yangu mdogo akatoka Muscat kuja kunichukua.Jina lake ni Abdulla bin Habiib bin Salim Alraawahy.
Jibu : Ni Michungwa miwili.Baada ya muda huo baba yangu mdogo akatoka Muscat kuja kunichukua.Jina lake ni Abdulla bin Habiib bin Salim Alraawahy.
Tukaenda mpaka Oman nikakaa miaka niliyokaa.Wengine wanasema nilikaa miaka 14 au 15.
Swali:Ulipotoka kule Oman kurudi Unguja mlitumia usafiri gani?.
Jibu:Usafiri tuliotumia ni jahazi.Sembuku moja ya watu wa Samail baatin huko Udama.Huyo nahodha jina lake Yussufu.
Nakumbuka
siku hizo hakuna riali,ilikuwa inatumika kursh.Nililipa kursh
saba,nikapewa kikaratasi tu.Hakuna siku hizo kupiga picha na nini na
nini !,hakuna wakati ule.
Siku zile mtawala wa Oman alikuwa sayyid Said bin Taimuur.Akasema sayyid Said hapa pana gunia saba za zabibu zinahitaji kupakiwa zipelekwe Dhofar halafu nyie mwende zenu.Tukapakia.
Dhofar ndiyo hii sasa inayoitwa Salala na mfalme Qaboos.
Tulipofika tukateremsha nikaulizwa wee mtoto mdogo wenda wapi?.Nikasema Yaa sayyid anaa adh-habu ilaa daar Zinjibaar.Nikajibishana nao kwa kiarabu kujitetea kuwa baba yangu amefariki na mama yangu yuko Zinjibaar.
Mwishowe nikaruhusiwa.Nikaambiwa;Marhaban bika.Hayya idh-hab yash-haduka Rahmaan.
Tukatoka
moja kwa moja mpaka tukafika Zanzibar.Kufika sikukaa sana nikaenda
mpaka Tabora kumtizama mama yangu.Nikamkuta bado mama yu hai.
0 comments:
Post a Comment