DAR ES SALAAM.
MPIRA alioucheza Rais Barack Obama wa Marekani mwishoni mwa ziara yake hapa nchini, ambao una uwezo wa kuzalisha umeme, utasambazwa vijijini na kuwa chanzo cha nishati mbadala.
MPIRA alioucheza Rais Barack Obama wa Marekani mwishoni mwa ziara yake hapa nchini, ambao una uwezo wa kuzalisha umeme, utasambazwa vijijini na kuwa chanzo cha nishati mbadala.
Mpira huo aliuchezea Rais Obama na kumpasia Rais
Kikwete ikiwa ni sehemu ya kuitangaza teknolojia hiyo mpya hapa nchini,
walipokuwa kwenye eneo la mitambo ya kuzalishia umeme ya Kampuni ya
Symbion, Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Kitendo cha Rais Obama kucheza mpira huo hapa
nchini kiliashiria kwamba Marekani inatarajia kuing
iza teknolojia hiyo hapa nchini na wakati wowote itaanza kutumika hasa kwa maeneo ya vijijini ambako hakuna mtandao wa umeme.
iza teknolojia hiyo hapa nchini na wakati wowote itaanza kutumika hasa kwa maeneo ya vijijini ambako hakuna mtandao wa umeme.
Teknolojia hiyo imekuja wakati ambapo Serikali
imekuwa katika mkakati wa kuusambaza umeme kwa awamu katika maeneo
mbalimbali ya vijijini, kupitia kwa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Serikali imekuwa ikitekeleza mradi wa REA kwa
ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Kukabili Changamoto
za Milenia (MCC).
Mpango wa REA umekusudiwa kuvijengea vijiji uwezo
na kuwa na mazingira mazuri yakiwemo ya uwekezaji na ujenzi wa viwanda
vidogovidogo na kuzima wimbi kubwa la vijana kukimbilia mijini kutafuta
kazi. Ofisa wa Mawasiliano wa Symbion, Julieth Foster aliliambia
Mwananchi Jumapili kuwa kilichofanywa na Rais Obama ni uzinduzi wa
kuitangaza teknolojia hiyo nchini.
Alisema mpango wa kuitangaza teknolojia hiyo uliandaliwa na taasisi ya Marekani inayojulikana kama Unchartered, ambayo kwenye tovuti yake imesema itaanza kusambaza mipira hiyo sehemu mbalimbali duniani kulingana na watakaoiagiza.

Kulingana na utaalamu wa utengenezwaji wake, mpira huo unapozunguka, unazungusha ndani mashine ya kuzalisha umeme.
Makadirio ya awali, mpira huo utauzwa kati ya Dola
za Marekani 125 hadi 150 ambayo ni sawa na wastani wa kati ya Sh200,000
hadi 250,000.
Hata hivyo, kwa hapa nchini huenda mipira hiyo
ikauzwa kwa bei ya chini zaidi ya ile ambayo imetangazwa kwenye tovuti
hiyo ya Unchartered.
Hii inatokana na ukweli kwamba mradi wa kusambaza
mipira ya namna hiyo barani Afrika upo chini ya Mfuko wa Misaada wa Rais
wa zamani wa Marekani, Bill Clinton.
Gazeti la Marekani la Washington Post liliandika
wiki hii kuwa teknolojia hii imekuwa ikiendelezwa na marais wa Marekani,
kupitia miradi ya kusaidia matatizo ya umeme katika Bara la Afrika.
Mtandao mwingine ukaeleza kuwa matumizi ya
teknolojia hiyo kwa Afrika yamekuwa ni moja ya ajenda za Mfuko wa
Misaada wa Clinton unaoendesha shughuli zake dunia nzima.
CHANZO MWANANCHI.
CHANZO MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment