Suali:Alikuwa anaitwa nani vile?.
Jibu:Anaitwa Zuhura bint Shorichoma Mnyasamba,kabila yake Mmanyema.
Swali:Na hapa Tongoni ulifikaje?.
Jibu:Nilipotoka Tabora nikaja Darisalama.Nikafanza kazi Ridoch Motors kwa muda mfupi sana.Nikaona mambo yenyewe si mazuri sana.
Nilikuwa
nasikia siku zote Tanga,Tanga !.Nikasema kwa nini nisiende Tanga
nikakuone kukoje?.Nikapita kwa njia ya pwani,njia ya Bagamoyo kwa siku
mbili na nusu.
Swali:Ulitumia usafiri gani?.
Jibu:Kwa miguu.
Tukatoka Kiriki jogoo la kwanza.Nilikuwa nikikaa na mama yangu mdogo akiitwa Nuuri bint Shorichomba.
Nikaja moja kwa moja mpaka sehemu moja inaitwa Ununio .Baada kufika Ununio tukakata njia.Pana njia ya mkato .
Swali:Ulikuwa wewe na nani?.
Jibu:Kijana
mmoja akiitwa Sakira,kijana wa kisukuma.Tukaongoza moja kwa moja mpaka
Bagamoyo.Tukafika saa 11.30.Tukala chak
ula katika hoteli ya kijana mmoja
anaitwa Ibrahim.Kabila yake Bulushi.Tukalala pale.
Tukavuka
njia yetu Kisauke,tukaja moja kwa moja mpaka Saadani.Baada ya kufika
Saadani tukatoka moja kwa moja bila kukaa pahala mpaka Mkwaja,saa mbili
kasoro usiku.Tukalala Mkwaja.
Siku ya pili tukaondoka tukaifuata njia ya Pangani.Tulikwenda mwendo mkubwa mpaka tukafika sehemu moja inaitwa Sakura.
Kwa bahati tukapata gari iliyokuwa ikisomba marobota ya katani ikatuchukua moja kwa moja mpaka Pangani.
Pale palikuwa na mjomba wangu mmoja akiitwa Suleimana bin Juma,maarufu akiitwa Suleiman Mtesi.
Swali:Jee ulikuwa ukijuwana naye kabla?.
Jibu:Laa!,ilikuwa simjui,nilikuwa nikiambiwa tu kuwa kuna mjombao Pangani.Lakini sikubahatika kumfuata.Nilipofika nikamuulizia nikampata.
Swali:Unakumbuka huo ulikuwa ni mwaka gani?.
Jibu:Kwa kweli bwana sikumbuki ilikuwa ni mwaka gani.Siku zimekuwa nyingi sana.
Nilibakia pale siku kidogo halafu nikatoka kimatembezi nikafika hapa Saadani.Pakanipendeza sana.
Swali:Jee jina la Saadani ya hapa limehusiana vipi na lile la Pangani?.
Jibu:Ndio limetokana na Saadani ya Pangani.Alilianzisha mwarabu mmoja kabila lake Al Bimaany.Akiitwa Swaleh bin Juma.
Swali:Tuendelee na hiki.
Jibu:Nilipofika
hapa nikaangalia mji wake ukanipendeza.Nikarudi Pangani halafu nikarudi
Zanzibar.Sikukaa sana,nilikaa kiasi y miaka miwili tu.Niliporudi hapa
nikakuta mabadiliko.Niliowakuta mwanzo sikuwakuta tena.
Nikakaa kitako kuangalia kazi za watu wa hapa.Nikaona ni mbili tu.Kulima na kuvua.Mimi nikashawishika sana na kazi ya kuvua.
Nikaingia
kuanza kuvua.Tangu ilikuwa sijui kuvua mpaka nikaitwa mimi
nahodha.Tangu ilikuwa navua kwa mishipi midogo mpaka nikawa navua kwa
mishipi mikubwa.
Nikaendelea na kazi hizo mpaka nikapokea cheti cha uvuvi.
Swali:Wakati
tukipinda kuja hapa,pale barabarani tulikuta bao lina tangazo kuwa eneo
hili la Tongoni linahifadhiwa kihistoria na serikali.Ni kitu gani hasa
kinachohifadhiwa?.
Jibu:Wakati
wa zamani walikuja watu wanatokea sehemu za Shirazi.Mmoja anaitwa Faki
Jaafar na mwenzake Mboza Ally.Walifika sehemu moja panaitwa
Mkongomani.Mimi sipajui.
Baadae Faki Jaafar alikuja kukaa hapa na Mboza Ally akaenda sehemu moja inaitwa Raninga,Kisimatui.
Wakakaa mpaka Mwenyezi Mungu akawajaalia wakazalia
wana wao.Na wengine washirazi wakaka Unguja sehemu moja panaitwa
Bwejuu.Na sehemu moja watu wa ukoo huo huo wakaka anaitwa Hamdan.
Swali:Tuendelee na historia ya hapa Tongoni.
Jibu:Nilipofika hapa
kupaangalia palivyo nikakuta ule mlingoti wa wajarumani bado ungalipo
kando kando ya bahari.Pia palikuwa na msikiti wa waarabu wa
Ibadhy.Msikiti upo mpaka leo lakini umekuwa haufai
kutumia,umeshavunjika.Bahari imekula.Hata palipokuwa na mlingoti wa
wajarumani huwezi kujua wapi. Ilikuwa ni ofisi ya serikali ya
kijerumani.Ilikuwa ni boma hasa,kambi ya jeshi.
Swali:Ni watu gani maarufu uliowakuta hapa Tongoni na Saadani ?.
Jibu:
Kusema kwa ukweli niliwakuta wazee wengi,lakini sasa nimekwisha
kuwasahau.Nawakumbuka akina Saleh Fakih,kina Waziri Aweya,skh Jumbe wa
Toba.
Swali:Tumepata taarifa kuwa mfalme wa Oman,sultan Qaabus bin Said amevutiwa sana na mashairi yako.Alikujuaje?.
Jibu:Ulipofika
ule ujumbe ulioletwa kuangalia jamaa wa kiarabu wa kizamani,ulipofika
Tanga ukauliza ukaambiwa yupo mzee wetu anaitwa Abdullah Mohammed anakaa
hapa Tongoni.Wakasema sisi tunapenda kukutana naye mzee huyo.
Mimi
nikaletewa habari na Salim bin Ally kuwa kesho kuna wageni wanakuja
kukutizama.Nikasema InshaAllah.Nikakaa kitako kuwasubiri mpaka saa
4,nikajiona nimechoka nikataka kuondoka,mara nikaona gari inakuja.
Tukaanza
kusalimiana nikawauliza waarabu nyinyi mnatoka wapi?.Wakasema tunatoka
Muscat,Oman.Nikawauliza kweli mnatoka Oman nyinyi?.
Nikawauliza
kweli mnaijuwa Oman nyinyi? au tapeli tu.Nikawauliza tena mnaijua Oman
au watembezi tu mliokwenda Oman?..Wakasema sisi ni wazaliwa hasa wa
Oman.
Nikawaambia nitawaulizeni maswali.
"Tumetoka
Afrika tumekuja kwa baharini.Tukiteremka tu tunakanyaga mchanga
Khurbamba.Tunateremka tunakuta kwa kulia Khur Al Wadia.Maujud?.Bado ipo?.
Nikawauliza tena.Kwa mkono wa kushoto suuq samak.Maujud?.Wakajibu maujud .Nikawaambia Anaa daakhil qaliil…..
0 comments:
Post a Comment