BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MOYO WA MZEE NELSON MANDELA ULISIMAMA NA KUSHINDWA KUFANYA KAZI KWA DAKIKA 40.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEaoOxUGO6PCPvKo-e9qwy03xNv_XAJYIv-S9weDRSsMx5v3BM3Sk3t2ZLwYcgbZUGR_xa8LxPvt4TlchngbY6Yh57ZUmo9rAR1d8Y-jP07kYf3Sp_qOUUY06Oq6s4OPOxZHQgXc1pSzg/s400/mandela.jpg 
JOHANNESBURG. 
KUHARIBIKA kwa gari la wagonjwa lililombeba Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, kulisababisha moyo wa shujaa huyo kusimama kwa dakika 40.
Hayo yalibainishwa na daktari wa moyo anayemtibu shujaa huyo wa Afrika Kusini, kwamba Juni 8, mwaka huu, wakati akipelekwa hospitali gari lililombeba lilipata hitilafu njiani na kukwama kwa muda.
Daktari huyo wa moyo anayeheshimika nchini Afrika Kusini, (jina linahifadhiwa) alisema jana kuwa gari la wagonjwa lililokuwa likimpeleka Mandela hospitali lilih
aribika katika njiapanda ya Gauteng na kusababisha wasubiri gari lingine kwa zaidi ya dakika 45.
“Moyo wake ulisimama kabisa tukiwa ndani ya gari, ikatubidi tumfufue kwa mashine (resuscitate),” alithibitisha daktari huyo bingwa.
Ripoti inaeleza kuwa gari hilo la wagonjwa linalomilikiwa na jeshi, liliharibika wiki tatu zilizopita kati ya Pretoria na Johanersburg.
Chombo cha habari cha Marekani, CBS kiliripoti jana kuwa moyo wa Mandela ulisimama kwa dakika kadhaa kabla gari lingine halijaletwa na kumpeleka Mandela katika hospitali ya Medi-Clinic.
Wakati moyo wa Mandela uliposimama, nje kulikuwa na baridi kali kiasi cha nyuzi joto sita tu, hali ambayo inaelezwa kuwa ilichangia kuharibu zaidi mapafu ya Baba wa Taifa la Afrika Kusini.
“Mke wa Mandela, Graca Machel, alikuwa amechanganyikiwa kwa dakika hizo 40, ambazo tulikuwa tukisubiri gari lingine,” kilisema chanzo hicho.
Ingawa msemaji wa Rais Jacob Zuma, Mac Maharaj alisema kuwa madaktari wamethibitisha kuwa Mandela hakupata madhara makubwa kutokana na baridi hiyo, madaktari wengi wameonyesha kupingana naye.
Daktari wa moyo, David Janekelow alisema, kutokana na hali yake, ucheleweshaji wa aina yeyote ile lazima ulisababisha madhara.
“Unahitaji kupata matibabu ya dharura haraka iwezekanavyo.

Kama mtu tayari alikuwa anafufuliwa, ucheleweshaji wa kumpeleka hospitali lazima ulete madhara,” alisema Janekelow.
Daktari mwingine wa moyo, Richard Nethonde alisema, Mandela angekufa pale barabarani wakati wanasubiri gari la wagonjwa liletwe, imekuwa ni kama bahati hakufa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: