BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTOTO WA MKULIMA MIZENGO KAYANDA PETER PINDA KUPANDISHWA KIZIMBANI ALHAMISI KISA KAULI YA KUWARUHUSU ASKARI KUPIGA RAIA....!!!.

Waziri mkuu pinda.

Pasiance mlowe mtafiti wa kituo cha sheria na haki za binadamu  akizungumza na waandishi habari jijini dar es salaam

     
    kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania kimetangaza rasmi kumpandisha mahakamani siku ya alhamisi waziri mkuu wa Tanzania mh Mizengo Pinda kufuatia kauli yake aliyoitoa bungeni mnamo mwezi wa sita kauli ambayo ilipingwa na watu wengi sana

          Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mkurugenzi wa maboresho na utafiti bw Harold Sungusia amesema kua uamuzi huo umekuja baada ya kuona juhudi za kumtaka waziri pinda kuwaomba watanzania radhi kugonga mwamba kitu ambacho amesema kuwa ni kitendo ambacho kimeashiria kupania.

           Bw Sungusia amesema kuwa siku ya alihamisi wanawasilisha kesi ya kumstaki waziri mkuu katika mahakama ambayo bado hawajaiweka wazi kwa wanahabari

          Kama utakumbuka wakati wa vurugu za arusha na zile za mtwara waziri mkuu akitoa kauli kuwa ,ukufanya fujo na umeambiwa usifanye fujo utapigwa tu,na mimi na sema wapigeni maana tumechoka.

Arold Sungusia mkurugenzi wa maboresho na utafiti  kituo cha sheria na haki za binadamu.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: