Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Tabora mstaafu amefariki
Dunia baada ya kujinyonga akiwa chumbani kwake Mjini Tabora.
Mwenyekiti
huyo Jaffary Ally, aliyekuwa miongoni mwa waasisi wa TANU Mkoani
Tabora,amejiua akiwa nyumbani kwake katika eneo la Ip
uli Manispaa ya Tabora. Sababu za kujiua bado hazijulikani.
uli Manispaa ya Tabora. Sababu za kujiua bado hazijulikani.
Mzee Ally anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 80 na alikutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia waya wa simu.
Inaelezwa
kuwa Mke wake ndie aliyekuwa wa kwanza kumkuta amejinyonga majira ya
saa kumi jioni juzi na kutoa taarifa kwa majirani akipiga mayowe.
Kwa mujibu wa majirani wa mzee huyo,inaelezwa hakuwa nyumbani kwake bali kwa mmoja wa watoto wake baada ya
kupata ajali ya pikipi na kulazwa kwa wiki moja katika Hospitali ya Mkoa Tabora,kitete.
Marehemu alijinyonga siku moja tu baada ya kuwasili nyumbani kwake tukio ambalo limewashangaza wananchi kwani alikuwa bado ni kiongozi.
Marehemu hadi nafariki alikuwa ni Mwenyekiti wa wazee wa Kata ya Ipuli na Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere yalipo makazi yake.
Marehemu Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora,Moshi Omary Nkonkota,alisema marehemu aliwahi kushika wadhifa alionao miaka ya nyuma huku akiwa bado ni tegemeo kwa Chama cha Mapinduzi na kusikitishwa na lililotokea.
Polisi Mkoani Tabora limeeleza linachunguza kifo hicho ili kujua chanzo cha hatua iliyochukuliwa na marehemu.chanzo rashidjuma,blogspot.com
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment