BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UGANDA YAIONDOA TANZANIA MASHINDANO YA CHAN 2013 KAMPALA KWA JUMLA YA BAO 4-1.


TIMU ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) imeaga rasmi mashindano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) baada ya kukubali kipigo cha bao 3-1 katika ardhi ya Uganda.

Mchezaji Kalanda Frank ndiye aliyanza kufungua panzia ya mabao kwa upande wa Uganda kwa bao lake la kuong
oza kabla ya kiungo mshambuliaji wa Tanzania, Amri Kiemba ksawazisha na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu ya bao 1-1.

Kipindi cha pili dakika ya tatu Uganda walifanya shambulizi langoni mwa Stars na kufanikiwa kuongeza bao la pili lililowekwa kimiani kwa njia ya mkwaju wa penalti na Brian Majwega  baada ya mchezaji wa Stars kunawa mpira eneo la hatari.

Ivan Ntege ndiye aliyeshindilia bao la tatu la The Cranes na kufanya Uganda kuongoza kwa bao 3-1 huku ikiiondoa Tanzania katika michuano hiyo kwa idadi ya jumla bao 4-1 baada ya mchezo wa mwanzo uliofanyika wiki zilizopita jijini Dar es Salaam Uganda kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa Taifa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: