MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri nchini Tanzania (TEF), "Absalom Kibanda" amesema
zipo taarifa mbalimbali za kutaka kupotosha ukweli kuhusu yeye, lakini
ukweli utabaki kuwa kweli na tukio alilofanyiwa ni la kihalifu,
linalotokana na misimamo ya kazi yake.
Aidha
amesema kabla ya kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya alikuwa muoga sana na
kwamba hakupata kujua kama yeye ni jasiri kwa kiwango hicho.
Kibanda
alisema hayo jana wakati akizungumza Dar es Salaam katika kipindi cha
Jenerali On Monday na kuongeza kuwa kalamu yake ndiyo iliyomfikisha hapo
na kwamba bado atajisemea mwenyewe huku akisema kweli daima.
Kibanda
ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari Limited (2006), alijeruhiwa
vibaya katika mk
asa uliotokea Machi 6, mwaka huu na kumwacha na ulemavu wa jicho, kidole na mifupa kadhaa mwilini kuvunjika.
asa uliotokea Machi 6, mwaka huu na kumwacha na ulemavu wa jicho, kidole na mifupa kadhaa mwilini kuvunjika.
“Nilikuwa
muoga sana kabla ya kupatwa madhala haya, nilikuwa nikiwaza jambo mara
mbilimbili na sikupata kujua kama mimi ni jasiri kiwango hiki…kwani hata
maneno ya madaktari waliokuwa wakinihudumia yalinifariji kuwa hata
shinikizo la damu na sukari viko katika hali nzuri,” alisema Kibanda na kutaka uchunguzi zaidi ufanyike.
Alisema
zipo taarifa mbalimbali za kutaka kupotosha ukweli kuhusu yeye lakini
ukweli utabaki kuwa kweli na kwamba yapo mambo ambayo atayafanya tofauti
na ilivyokuwa awali.
“Katika
miezi mitatu niliyokuwa nikipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini zipo
lugha nyingi za kishabiki ziliandikwa…ni wakati wa kuchunguza kwa kina
na kusema ukweli,” alisema Kibanda na kuongeza kuwa leo (jana) ni siku
100 tangu alipofanyiwa tukio hilo, lakini hakuna aliyekamatwa wala
kufikishwa mahakamani.
Kuhusu kupata ushirikiano katika shauri lake,
alisema amekuwa akipata mawasiliano kutoka kwa viongozi mbalimbali
wakiwemo pia viongozi wa ulinzi na usalama wa Taifa ambao wanachunguza
suala hilo.
“Maofisa
wa polisi wamekuwa wakiwasiliana nami na hata nilipokuwa Afrika Kusini
Jeshi la Polisi lilimtuma ofisa wake na alifanya mahojiano nami kuhusu
tukio hili,” alisema Kibanda na kusisitiza kuwa ifikie wakati serikali
iwe inajali pindi yanapotokea matukio ya aina hiyo.
Aidha
alisema tukio alilofanyiwa ni la kihalifu na anaamini kuwa aliumizwa kwa
misimamo yake ya kazi, lakini bado anatoa wito kwa wadau mbalimbali
kuendelea kuchunguza tukio hilo.
Kibanda alisema yapo mambo ambayo yalipindishwa kuhusu tukio hilo na kwamba atajisemea mwenyewe.
Akihitimisha
kipindi hicho, Muandaaji, Jenerali Ulimwengu alisema matukio kama hayo
yanapotokea yana tabia ya kukua, kusambaa na mwishowe kuota meno marefu
na kuyaondoa huwa hayawezekaniki tena, hivyo matukio kama hayo yazuiwe
yasijirudie.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment