![Abiria wakishuka kwenye ndege ya Jubba Airways, ndege ya kwanza kufanya safari za kibiashara kwenda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden Adde wa Mogadishu tarehe 30 Julai 2006, baada ya kufungwa kwa miaka 11. [Stringer/AFP]](http://sabahionline.com/shared/images/2013/05/16/somalia-flight-airspace-340_227.jpg)

Rais huyo hakujeruhiwa kwenye tukio hilo na hakukuwa na taarifa ya majeruhi yeyote.
Msemaji wa serikali Abdirahman Omar Osman alisema ndege hiyo iliondoka uwanja wa ndege wa Mogad
ishu saa tatu asubuhi lakini ilirudi mji mkuu baada ya kiasi cha dakika 20 za kukaa angani hitilafu ilitokea kwenye moja ya injini za ndege hiyo.
Afisa wa uwanja wa ndege aliiambia VOA kwamba ndege hiyo ilipata pancha wakati wa kutua Maafisa wa uwanja wa ndege wamekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba ndege hiyo ilishika moto.
Rais huyo na ujumbe wake walikuwa wakielekea Sudan Kusini kwa maadhimisho ya sherehe za uhuru wa nchi hiyo.
Kundi hilo baadae lilipanda ndege nyingine na kuendelea na safari ya Sudan Kusini.
0 comments:
Post a Comment