
DAR ES SALAAM.
MABADILIKO ya ratiba za mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi yanayoanzia safari zake Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo (UBT), yamesababisha abiria wengi kushindwa kusafiri huku wengine wakiagizwa kwenda Kimara mwisho.
Mwananchi iliyofika Kituo cha Mabasi Ubungo saa
11:30 asubuhi, ilielezwa na mmoja wa wafanyakazi wa mabasi ya Air
Force, Ipyana Mwamlenga, kuwa waliagizwa na Sumatra kuhakikisha mabasi
yote yawe yameondoka kituoni hapo ifikapo saa 1:00 asubuhi.
“Tuko katika mchakamchaka, tunatakiwa kuondoka
hapa hadi saa 1:00 asubuhi ...unajua tulishaamua kuwa hakuna usafiri leo
kutokana na barabara kufungwa, lakini tukaamua tuondoke nyuma ya muda
wa kawaida,” alisema.
Gazeti hili lilishuhudia idadi kubwa ya mabasi
yakitoka kituoni hapo kuanzia saa 12:30 asubuhi, huku ask
ari wa usalama barabarani wakihimiza madereva kuondoka haraka ili wasilete usumbufu barabara itakapofungwa.
ari wa usalama barabarani wakihimiza madereva kuondoka haraka ili wasilete usumbufu barabara itakapofungwa.
Baadhi ya abiria walionekana kupigwa butwaa baada ya kukuta mabasi waliyotakiwa kusafiri nayo kuondoka.
“Wasubuiri hawa wanakuja huko, wote wana tiketi,”
alisikika mwanamke mmoja akiwasiliana na wahusika wa mabasi ya Prinses
Muro, lililoondoka mapema.
Habari zilizopatikana jana asubuhi kituoni hapo,
abiria waliokuwa wasafiri kwa mabasi yanayoanzia safari zake zaidi ya
saa 1:00 asubuhi, walitakiwa kwenda Mbezi.
Hata hivyo, mabasi yaliendelea kutoka kituoni hadi saa 1:40 asubuhi.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani,
Mohamed Mpiga, alisema mabasi na malori yote yanayotoka mikoani
yatazuiwa Kibaha hadi saa 7:00 mchana.
Mpiga aliwataka wasafiri wanaoelekea mikoani kuhakikisha wanawahi kwa sababu ratiba za mabasi zilikuwa zimebadilika.
CHANZO MWANANCHI.
CHANZO MWANANCHI.

0 comments:
Post a Comment