RAIS mstaafu, Benjamin William Mkapa, ameonyesha wazi kutoridhishwa na
mwenendo wa matukio ya uvunjifu wa amani hivi sasa.
Mkapa, mmoja wa
viongozi ambao wanajiamini katika kauli zao, amewataka Watanzania
kutochoka kusali na kuiombea nchi ili amani iendelee kutawala. Alisema
jukumu hilo linawahusisha watu, wakiwamo viongozi wa dini ambao wana
dhamana kubwa kwa waumini wao.
Mkapa alitoa kuali hiyo jana mjini
Mwanza, muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi, katika jengo la
ghorofa nne la Chuo Kikuu cha Sayansi, Tiba na Afya, kinachomil
ikiwa na
Hospitali ya Bugando. “Watanzania tukitaka uchumi wetu ukue, lazima nchi
iwe na amani, bila hali hiyo hakuna chochote kitakachofanyika.
"Ndugu
zangu, nawaomba Watanzania wote kwa itikadi zao, tuwaombee viongozi
wetu wa dini ili wawe na ushirikiano mzuri...na wao waliombee taifa
hili, hii ni tunu tuliyopewa,” alisema Mkapa.
Pamoja na Mkapa kuzungumza kwa kifupi, alifichua siri nzito ambayo hajawahi kuitoa hadharani.
Siri
hiyo, ni ile ambayo alidai wakati akiwa mdogo, wazazi walitaka asomee
masomo ya upadri, lakini hakufanikiwa kufikia lengo hilo.
“Wazazi wangu walikuwa walitaka niwe padri, kwa bahati mbaya ndoto ya wazee wangu haikutimia,” alisema Mkapa.
Alisema
yeye anatambua Mungu alimpangia kuongoza Watanzania, jambo ambalo
lilitimia kwa kipindi cha miaka 10 ya kuliongoza taifa.
Habari
zaidi zinasema, jana jioni alitarajiwa kuongoza harambee ya kukusanya Sh
milioni 900, kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo la Chuo Kikuu cha
Sayansi, Tiba na Afya, ambayo itahudhuriwa na watu mbalimbali.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bugando, Profesa Jacob Mutabaji,
alisema fedha zitakazopatikana zitasaidia kazi ya ujenzi wa majengo
ambayo yamegharimu Sh milioni 400.
Alisema kama jengo hilo likikamilika, litapewa jina la Mwalimu Nyerere na litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,400.
Juzi,
Rais Jakaya Kikwete wakati akifunga kongamano la amani lililoandaliwa
na Kituo cha Taasisi ya Demokrasia Tanzania (TCD), alikiri kuwapo na
viashiria vya uvunjifu wa amani nchini.
Alisema katika siku za
karibuni, kumeibuka viashiria vingi, vikiwamo vya watu kutangaza
kuanzisha vikundi vya mgambo kwa ajili ya kujilinda.
CCM
Katika hatua nyingine, Mkapa vijana kudumisha amani na mshikamano uliopo
Akizungumza
na viongozi na watumishi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza,
alipofika kusaini kitabu cha wageni, alisema amani ndiyo tunu ya taifa.
Mkapa
alipokelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga ambaye
aliwatambulisha watendaji na watumishi na kutoa maelezo ya hali ya
kisiasa ilivyo mkoani humo.
Aliwapongeza na kuwataka kuendeleza
mshikamano na umoja ndani ya chama ili vijana wasipotoshwe na wasiasa
wanaotaka madaraka kwa hila na kuleta machafuko nchini kwa lengo la wao
kukimbilia Ikulu kushika madaraka makubwa ya nchi, wakati bado wachanga.
Mkapa
alimwagia Mbunge wa Bariadi Magharibi,John Cheyo (UDP) kutokana na
kauli aliyoitoa kwenye semina ya kongamano la amani lililoandaliwa na
Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD), aliposema kikosi kipya kinachotaka
uongozi wa Taifa hili kina wajibu wa kujifunza.
Mkapa akinukuu
maneno ya Cheyo, alisema “kikosi kipya kinachotaka madaraka hakielewi na
hakitaki kukili kwamba taifa hili na nchi hii inahistoria, mira na tunu
zake za kutawala .
“Kwa kweli tusiombee wapinzani hawa washike
nchi hawafai na haifanani kabisa na kauli, lugha na matendo
yao,wanadhani wakishika madaraka makubwa ya nchi hii itasitawi zaidi
kuliko ilivyo kwa CCM? Si kweli hata kijiji hawajaweza kutawala na hata
hivyo wanavyotawala na majimbo hali yake ni ya hovyo”alisema
“Kizazi
kipya hakitaki kukiri na kutambua kama nchi hii ina historia, mira,
desturi zake na hata tunu za kutawala, ni vyema wakalitambua na
kujifunza badala ya kuanza kuivuruga amani, umoja na utulivu kwa lengo
la kukimbilia kushika madaraka makubwa. CHANZO MTANZANIA
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / RAIS MSTAAFU AWAMU YA TATU, BENJAMIN WILLIAM MKAPA ASHTUSHWA NA HALI YA AMANI NCHINI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment