DAR ES SALAAM.
Siku tatu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuponda mpango wa Chadema kuanzisha kambi kwa ajili ya mafunzo ya ulinzi kuwalinda viongozi na wanachama wake, chama hicho kikuu cha upinzani nchini kimeibuka na kusema kuwa kinaendelea na mpango huo na kambi hizo zitaanza rasmi wiki ijayo.
Siku tatu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuponda mpango wa Chadema kuanzisha kambi kwa ajili ya mafunzo ya ulinzi kuwalinda viongozi na wanachama wake, chama hicho kikuu cha upinzani nchini kimeibuka na kusema kuwa kinaendelea na mpango huo na kambi hizo zitaanza rasmi wiki ijayo.
Kimesema hakitishwi na kauli ya Jeshi la Polisi
kukionya juu ya uanzishwaji wa mafunzo hayo, kwamba jeshi hilo
linatakiwa kuanza kukizuia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwanza, kwa
maelezo kuwa chama hicho tawala pia kina kikundi cha ulinzi ‘Green
Guards’ ambacho kinafanya mafunzo ya kijeshi, huku kikitumia silaha za
moto.
“CCM ndiyo wataipeleka nchi hii pabaya,
wanawafundisha vijana huku wakiwabebesha bunduki, wanajenga taifa la
aina gani, bunduki ni silaha ya kivita sasa wanaandaa watu kupigana na
nani” alisema Mkurugenzi wa Organaizes
heni na Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaira jana wakati akizungumza na wanahabari huku akionyesha picha za mafunzo ya CCM, zinazoonyesha vijana wakiwa wamebeba silaha (hata hivyo ni mbao zilizotengenezwa kwa mfano wa bunduki).
heni na Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaira jana wakati akizungumza na wanahabari huku akionyesha picha za mafunzo ya CCM, zinazoonyesha vijana wakiwa wamebeba silaha (hata hivyo ni mbao zilizotengenezwa kwa mfano wa bunduki).
Wakati Chadema wakieleza hayo, CCM kimeshtushwa na taarifa hizo na kueleza kuwa hali hiyo sasa inahatarisha usalama wa nchi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho
(UVCCM), Martin Shigela alisema ni vyema Chadema kikawaambia wananchi
wawalinde, kuliko kuanzisha mafunzo huku akimtaka Msajili wa Vyama vya
siasa nchini, John Tendwa kulitizama kwa kina suala hilo.
Akifunga Kongamano la Amani lililoandaliwa na
Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Dar es Salaam Julai 10, mwaka huu,
Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa pia alikosoa kitendo
cha Chadema kususia kongamano hilo alisema, “Sasa hawa kweli wanapenda
amani yetu wakati hawapendi tuzungumze wanataka watu wauane, wapigane.”
Mbali na Rais Kikwete, Msemaji wa Jeshi la Polisi
nchini, SSP Advera Senso juzi alikionya chama hicho kuhusu mpango huo
akisema kuwa kitendo cha chama chochote cha siasa kikiwemo Chadema,
kuanzisha kikundi cha kujihami ni kinyume na sheria za nchi na endapo
watafanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kauli ya jana ya Chadema ni mwendelezo wa ile
iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe Julai 9, mwaka
huu, ambapo alisema kimechukua hatua hiyo baada ya Serikali na vyombo
vyake vya ulinzi na usalama kushindwa kufanyia kazi malalamiko yao
kuhusu mauaji, vitisho na matukio ya kutisha wanayofanyiwa baadhi ya
viongozi na wanachama wao.
Katika ufafanuzi wake Kigaila alisema Chadema
hakianzishi vikundi vya kijeshi, bali mafunzo ya kuwafundisha walinzi
wa chama hicho ‘Red Brigade’, jinsi ya kujilinda.
“Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ni haki kwa raia yeyote kujilinda, Chadema ni taasisi ni haki
yetu kuilinda taasisi yetu ndiyo maana tumesajili kikundi chetu cha
ulinzi, sasa nani anatutisha, tunataka polisi waanze na CCM kwanza ambao
katika mafunzo yao wanafundisha hadi kupiga saluti na kutumia silaha,”
alisema.
Alisema mafunzo hayo yataanza rasmi wiki ijayo,
huku akisita kutaja siku yatakayoanza, wala mikoa yatakayofanyika na
kusisitiza kuwa hayo yatatangazwa wiki ijayo wakati vijana wakienda
katika mafunzo. CHANZO MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment