Said Juma Makamba akiwa hospitalini baada ya shambulio hilo juzi. |
Shekhe
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa
kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi
usiku akiwa nyumbani kwake jijini Arusha.
Shekhe
Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya
Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni,
kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu.
Akizungumza
kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa
kuamkia jana nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala
baada ya kutoka kuswali Swala ya Tarawei.
Shekhe Makamba ambaye pia ni
Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema baada ya swala hiyo
alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana wawili ambao walikuwa
wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake ili kulala.
Alisema hata hivyo, kabla ya
kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba wakati akirudi
ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla alimuona mtu akiwa
amesimama jirani na mlango.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment