Meneja
wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe (Katikati) akionesha sehemu ya
vifaa walivyokabidhi leo kwa klabu za Simba na Yanga kwa ajili ya msimu
mpya wa Ligi Kuu Bara 2013/2014, kushoto ni Katibu Mkuu wa Sim
ba Evodius
Mtawala na Kulia ni Katibu Mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako.Katibu wa Simba Evodius Mtawala (kushoto) na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe (kulia) wakiwa wameshika vifaa ambavyo Simba imekabidhiwa leo kwa ajili ya msimu wa ligi 2013/14 |
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe (kushoto) na katibu wa Yanga Lawrance Mwalusako (kulia) wakiwa wameshika vifaa ambavyo Yanga imekabidhiwa leo kwa ajili ya msimu wa ligi 2013/14 |
Ikiwa
ni sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi
vifaa vya michezo kwa klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC
kwa ajili ya msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwezi
ujao.
Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema
“Tunawapatia vifaa mapema kabla ya ligi kuanza ili wapate muda wa
kutosha kujiandaa kwa ajili ya msimu wa 2013/14 ambayo bila shaka
itakuwa na changamoto kubwa kwa timu hizi mbili na pia tunaam
ini kuwa siri ya mafanikio katika michezo ni maandalizi mazuri.
ini kuwa siri ya mafanikio katika michezo ni maandalizi mazuri.
Ni matumaini yetu
kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa Simba na Yanga wataiwakilisha Kili
vizuri na kufurahia kuzichezea klabu hizi kongwe.”
Kavishe
aliongeza kuwa Vifaa ambavyo leo tunatoa ni pamoja na mipira, viatu,
soksi, shin guards, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vitu
vingine vingi ambavyo vitawezesha timu hizi za Simba na Yanga kucheza
wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya juu.
Kilimanjaro
Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji
kinachoongoza katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba
uhusiano wetu na klabu hizi ni kiungo muhimu sana katika kuendeleza
mpira wa miguu hapa Tanzania. Tutaendelea kutimiza wajibu wetu kwa klabu
hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha tunalifikisha soka la
Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.
Kavishe
alisema kuwa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Simba na Yanga
umelenga kukuza soka la Tanzania, kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki
wengi wa mpira wakati na vilevile kuwaweka wachezaji wa Tanzania katika
nafasi nzuri ya kimataifa.
Tunawashukuru
viongozi wa Simba na Yanga, mashabiki wote, vyombo vya habari na wadau
wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea kupata kwenye udhamini
wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio ya uhusiano wetu na klabu hizi mbili
maarufu.
“Tunawaomba
mashabiki wa Simba na Yanga waendelee kuiunga mkono bia yao ya
Kilimanjaro Premium Lager kwani tunafanya kila jitihada kuwapa burudani
na kufikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.”
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment