Baadhi ya Wanahabari wakikusanya net ambazo walizikuta katika moja ya kijiji kilichopo karibu na ziwa Vctoria Kisumu nchini Kenya, net hizo ni maarufu kama kokoro ambazo kwa kutumia net hiyo wavuvi wamekuwa wakizoa mpaka mayai na hivyo kuyaharibu. Baadhi ya samaki ambao walikamatwa katika zoezi la Wanahabari la kukamata samaki ambao wamekuwa wakivuliwa katika ziwa Victoria kinyume cha sheria, Wataalamu wa masuala ya samaki wamese endapo hatua za kudhibiti uvuvi haramu hazitochukuliwa kunauwezekano mkubwa wa samaki kumalizika katika ziwa hilo.
Mmoja wa Askari Polisi akizungumza na wavuvi waliokutwa na net za
kuvulia samaki aina ya kokoro ambazo zimepigwa marufuku kutumika.
Wanahabari wakipakia katika gari samaki ambao wamevuliwa kinyume cha
sheria baada ya kufanya msako katika maeneo mbalimbali ya Kisumu zoezi
hilo lilifanyika usiku kucha na mchana Ziwani na Barabarani.
Wafanyakazi wa Wizara ya Uvuvi Nchini Kenya wakiwa wamebeba tenga la
samaki wadogo ambalo walilikamata katika zoezi maalumu ambalo
lilishirikisha Wanahabari kutoka maeneo mbambali ya Nchi za Afrika
waliokuwa katika mafunzo ya uvuvi wa samaki chini ya Smartfish kulia ni
Mwandishi wa habari kutoka Nchini Tanzania Bw Finegani Wasimbey (PICHA
NA IPSHA BLOG)
0 comments:
Post a Comment