Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dk. Michael Kadeghe akiwa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Mbozi Ally Wendo katika eneo la ajali leo asubuhi. |
TAARIFA
YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI -AJALI
MNAMO TAREHE 15.08.2013 MAJIRA
YA SAA 20:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI
CHA CHIMBUYABARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA
YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.765 BBA AINA
YA SCANIA LILILOKUWA LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA TUNDUMA
LILIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE
LILIGONGA TREKTAAMBALO HALIJAFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI KISHA
KULIGONGA GARI ACP 8839 AINA YA SCANIA MALI YA KAMPUNI
YA USAFIRISHAJI YA DHANDHO LILILOKUWA LIKITOKEA
TUNDUMA KUELEKEA MBEYA MJINI DEREVA WA GARI HILO BADO KUFAHAMIKA. KATIKA AJALI
HIYO WATU WATATU WAWILI KATI YAO WALIKUWA KATIKA GARI T.765 BBA
NA MMOJA NI DEREVA WA TREKTA AMBAO HAWAJATAMBULIKA MAJINA
WALA MAKAZI YAO, WOTE WANAUMEWALIFARIKI DUNIA PAPO
HAPO. AIDHA WATU WAWILI WALIOKUWA KATIKA GARI ACP
8839AMBAO PIA HAWAJATAMBULIKA
WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI
YA SERIKALI VWAWA WILAYA YA MBOZI. CHANZO CHA
AJALI KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Na Mkwinda
Blog
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment