Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akionyesha picha ya Msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari,masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko nchini Afrika Kusini hivi karibuni.
Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akiongea na waandishi
wa habari leo ofisini kwake jijini Dares salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na
Wizara ya Uchukuzi juu ya sakata la madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko Afrika
Kusini hivi karibuni.Dkt. Mwakyembe amewafukuza kazi mtandao mzima uliohusika
kusaidia kusafirisha madawa hayo, pia Waziri Mwakyembe ameliagiza jeshi la
Polisi kuwakamata wafanyakazi hao na kuwaunganisha na wenzao kujibu mashitaka
ya jinai.CHANZO MICHUZI BLOG
waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Uchukuzi
akiwa anafafanua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuushughulikia mtandao mzima
uliosaidia kupitisha madawa ya kulevya.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment