SIKU mbili baada ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea, jijini Dar es Salaam kunusurika kuteketea kwa moto uliotokana na milipuko ya mabomu, bomu lingine limekutwa kwenye uzio wa Kanisa hilo Usharika wa Kijitonyama.
MADAKTARI WAKIMPATIA HUDUMA YA KWANZA MAJERUHI WA MLIPUKO WA BOMA.
mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma
mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma
Hali hiyo ilizua taharuki kubwa kwa wakazi wanaioshi jirani na kanisa
hilo ambako pia kuna tawi la Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (Teku).
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia NIPASHE jana jioni, viongozi wa kanisa hilo walitoa taarifa polisi na ask
ari kufika eneo hilo ndani ya dakika kumi.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliliambia NIPASHE kuwa baada ya maofisa wa polisi kuwasili katika eneo hilo, walikuta bomu hilo halijalipuka na kuondoka nalo.
Kutokana hofu kuwa bomu hilo lingeweza kulipuka wakati wowote, baadhi ya wakazi eneo hilo walianza kuondoka katika makazi yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alithibitisha kukutwa kwa bomu hilo na kwamba limeanza kufanyiwa uchunguzi haraka.
Wambura alisema polisi walipewa taarifa saa kati ya saa 10:00 na 10:30 jioni kuwa kuna kitu kinachosadikiwa kuwa bomu kimewekwa karibu na kanisa hilo.
Alisema baada ya polisi kufika walichukuliwa na kukabidhi kwa wataalam kutoka vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kulifanyia uchunguzi ili kubaini lilikotengezwa.
“Uchunguzi wa kitu hicho kinachodaiwa kuwa bomu umeanza na taarifa itatolewa rasmi,” alisema.
Usiku wa kuamkia juzi kanisa hilo Usharika wa Segerea, jijini Dar es Salaam nalo lilinusurika kuteketea kwa moto uliotokana na milipuko ya mabomu .
Mabomu hayo matatu ya kienyeji yaliyorushwa ndani ya kanisa hilo na watu wasiofahamika, yalitengenezwa kwa chupa zilizojazwa mchanganyiko wa mafuta ya taa na petroli na kuwashwa moto.
Moto huo uliunguza eneo la madhabahu na sehemu kubwa ya gari la mchungaji wa kanisa hilo, Noah Kipingu.
Mchungaji Kipingu alikaririwa akisema kuwa chupa za bia zilizojazwa mafuta hayo zikiwa zimezibwa na mifuniko iliyotobolewa tundu la utambi ziliwashwa moto ili kuchochea milipuko.
Hata hivyo, alisema hakuna majeruhi wala vifo vilivyotokea kwenye mlipuko huo licha ya watu kukumbwa na taharuki.
Kadhalika, kanisa hilo lililojengwa kwa mbao na mabati lilinusurika kuungua pamoja na samani hasa viti vya plastiki, ala za muziki-ngoma, vipaza sauti na vifaa vya ibada kama mimbari ya kioo havikuathirika.
Alisema waumini zaidi ya 30 wakiwa wameshikana mikono kwenye mduara huku katika ibada ya mkesha wa kuombea mkutano wa Injili uliotarajiwa kuanza jana, walikumbwa na taharuki baada ya kusikia kishindo cha mlipuko kilichoambatana na moto.
Alisema watu wasiofahamika waliokuwa nje ya kanisa hilo, walirusha chupa tatu zilizopitia kwenye mtambaa wa panya na kuangukia ndani ya kanisa sehemu ya madhabahu na kuunguza kurasa chache za Biblia zilizokuwa zimefunguliwa, mto wa kupigia magoti, kipande cha sakafu ya altare na nyaya za spika.
Alisema bomu lingine lilitegwa chini ya gari lake kwenye tangi na lilipolipuka liliunguza. Mabomu hayo yalitupwa kati ya saa 7:45 na saa 8:00 usiku, kipindi hicho waumini Polisi na waumini huo walipokagua eneo la tukio waliokota chupa nyingine tatu ambazo hazijalipuka zikiwa zimetupwa na watu hao ambao hadi sasa hawajafamika.
Mchungaji huyo alisema hajui sababu ya mashambulizi hayo na hawezi kumtuhumu mtu yeyote kuhusika na tukio hilo.CHANZO: NIPASHE.
0 comments:
Post a Comment