Madini ya Tanzanite.
Habari zilizotufikia hivi punde Kutoka chumba chetu cha habari zinaeleza kuwa mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana kwa jina la Erasto Msuya na pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo, amepigwa risasi zaidi ya sita na watu wasiojulikana na kufa papo hapo.
Habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara.
Habari zaidi tuvute subra
kidoogo,tutazidi kufahamishana kadiri ya taarifa zitakapokuwa zikiingia.
Mungu ailaze roho ya marehemu
mahali pema peponi-Amen.
chanzo http://issamichuzi.blogspot.com

0 comments:
Post a Comment