Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera, Avelin Mushi.Hata hivyo, uamuzi wa chama hicho unaonekana kupuuza ushauri uliotolewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete, alioutoa hivi karibuni wakati wa ziara yake mkoani Kagera kwa kuzitaka pande zilizokuwa zinapingana kufikia maelewano.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya CCM mkoa, Katibu wa chama hicho Mkoa wa Kagera, Avelin Mushi, alisema jana kuwa uam
uzi huo umekuja kutokana na chama kujali maslahi ya wananchi tofauti ya watu binafsi.
Mushi aliwataja madiwani hao wanane kuwa ni Yusuph Ngaiza wa Kata ya Kashai ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Bukoba; Samuel Ruhangisa (Kitendagulo); Murungi Kichwabuta (Viti maalumu); Deusdedith Mutakyawa (Nyanga); Richard Gaspal (Miembeni); Alexander Ngalinda (Buhembe) ambaye pia alikuwa Makamu Meya; Dauda Kalumuna (Ijuganyondo) na Robert Katunzi wa Kata Hamugembe.
Hata hivyo, Mushi alisema Ngaiza ataendelea na wadhifa wake wa uenyekiti wa CCM kwa kuwa chama ngazi ya Taifa ndicho kinachoweza kulishughulikia suala hilo.
Katibu huyo alisema kuwa suala la kumvua uenyekiti Ngaiza limepelekwa ngazi ya juu zaidi maana mkutano huo hauna mamlaka ya kumvua wadhifa huo.
Mushi alisema kuwa kufukuzwa kwa madiwani hao ni kutokana na mgogoro ulidumu kwa muda mrefu na kuwahusisha Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki na Meya wa halmashauri hiyo, Dk. Anatory Amani.
Mushi alisema kuwa vikao vya chama vimekuwa vikiendelea kwa kufuata kanuni na taratibu kwa kuwaonya kutokana na tuhuma dhidi ya serikali na CCM kwa kushirikiana na madiwani wa kambi ya upinzani kutotekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi, lakini wahusika wote wamekuwa wakikaidi maagizo ya kuitwa kwenye vikao.
Mushi alisema chama ngazi ya mkoa kina mamlaka ya kuchukua uamuzi kilioufanya kuwatimua.
Katika mgogoro huo, baadhi ya madiwani wa CCM na wa upinzani walikuwa wakishinikiza Meya Amani atimuliwe kwa madai kuwa alikuwa anafanya ubadhirifu wa mali za halmashauri hiyo.
CHANZO:
NIPASHE

0 comments:
Post a Comment