BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CCM YAWAWASHIA MOTO WAZIRI KAGASHEKI NA MEYA WA MANISPAA YA BUKOBA NI SAKATA LA KUTIMULIWA KWA MADIWANI WA CCM.

 
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki akiwahi kuingia katika Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, Dodoma jana,alipokwenda kuhojiwa na Kamati Kuu ya chama hicho kuhusu mgogoro uliosababisha kuvuliwa uanachama kwa madiwani wanane wa Bukoba Mjini. Picha na Edwin Mjwahuzi.
  
DODOMA. 
WAKATI Kamati Kuu ya CCM imeamua kuumaliza mgogoro wa madiwani wake wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa kutoa onyo kwa viongozi wake, ndani ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), hakujatulia kwani kuna mpango wa kumwondoa Katibu Mkuu wake, Martin Shigela.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya vikao vya Kamati Kuu zimesema kwamba viongozi kadhaa wa chama hicho akiwamo Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamisi Kag
asheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani wameonywa kutokana na mgogoro wa muda mrefu katika wilaya hiyo.
Wengine waliotakiwa kupewa karipio ni pamoja na  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Costancia Buhiye na Katibu wake, Averin Mushi ambao walitarajiwa kuhojiwa jana usiku.
Habari kutoka ndani ya vikao hivyo vinavyofanyika Mjini Dodoma zilisema hata ule uamuzi wa kuwazuia Amani na Kagasheki kufanya siasa umeonekana unaweza kuleta athari kwao na kwa chama chenyewe, hivyo kuamua kutoa onyo na madiwani waliokuwa wamefukuzwa uanachama kuachwa kuendelea na nyadhifa zao. 

Vyanzo hivyo vya habari vilieleza kuwa suala hilo lilikuwa tayari limeamuliwa, isipokuwa ilikuwa ni lazima wahusika waitwe kufahamishwa uamuzi dhidi yao badala ya kusikia kwenye vyombo vya habari.
Hata hivyo, hadi jana wakati tunakwenda mitamboni ni viongozi wawili tu, waliokuwa wamehojiwa na Kamati Kuu ambao ni Buhiye na Mushi kwa kuwa tayari walikuwapo Dodoma wakiwa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu.
Balozi Kagasheki na Amani licha ya kwamba walikuwa wamewasili hapa, suala lao liliahirishwa kutangazwa kuwasubiri Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini, Yussuf Ngaiza na Katibu wa CCM Wilaya hiyo, Janeth Kayanda waliochelewa kufika mjini hapa baada ya gari lao kuharibika.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema uamuzi wa Kamati Kuu ungetolewa baada ya kumalizika kwa hatua ya kuwahoji viongozi hao jana.
Mgogoro wa Manispaa hiyo unatokana na miradi iliyopangwa na Meya Amani, ambayo inapingwa na baadhi ya madiwani wa CCM wa Manispaa akiwamo Balozi Kagasheki, ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii.
Hali ya siasa mkoani humo ilichafuka zaidi baada ya  Halmashauri ya CCM ya Mkoa wa Kagera kuwafukuza madiwani wanane kwa kosa la kumpinga Meya huyo na kupanga kumng’oa madarakani.
Madiwani hao ni Richard Gaspar (Miembeni), Murungi Kichwabuta (Viti maalumu), Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe) na Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendaguro), Dauda Kalumuna (Ijuganyondo) na Ngaiza(Kashai).
Hata hivyo, uamuzi huo wa kuwafukuzwa ulisimamishwa na Sekretarieti ya CCM ambayo ilisema kuwa Kamati Kuu ndiyo iliyokuwa na madaraka ya kutoa uamuzi wa mwisho dhidi yao na kuwataka kuendelea na kazi wakisubiri hatima yao.
Katika hatua nyingine, kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), ambacho kilikuwa kimalizike jana kimeongezewa siku moja zaidi na kitafungwa rasmi leo. MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: