Tukio
hilo lilitokea Juni 14, mwaka huu jijini Dar nyumbani kwao Mlandizi, Bagamoyo,
Pwani ambako mwanaume huyo alifunga ndoa na binti huyo na kurejea naye nyumbani
kwake, Ubungo Kisiwani, Dar huku baadhi ya watu wakih
ofia uhai wa ndoa hiyo.
Baada
ya kuanza maisha ya ndoa kama mke na mume, Agosti 6, mwaka huu taarifa zikafika
kwenye Kituo cha Polisi cha Ubungo ambapo maafande walisema hiyo haiwezekani.
“Polisi
walipopata habari walisema hakuna ndoa hapo, wakajipanga kwenda kuvamia
nyumbani kwa wanandoa hao,” kilisema chanzo.
Chanzo
kiliongeza kuwa, nje ya nyumba hiyo walimkuta msichana huyo anapika huku kaka
yake akiwa kajipumzisha ndani akisubiri lishe hiyo.
Kaizilege
alipobanwa alikiri kuwa mwanafunzi huyo ni mkewe walifunga ndoa ya Kiislamu,
Mlandizi. Kwa kuwa kisheria ni kosa kuoa mwanafunzi aliye chini ya miaka 18 alilazimikakupelekwa
Kituo cha Polisi, Magomeni, Dar.
Kwa
upande wake mwanafunzi huyo alikiri kuolewa na kaka yake. Alisema yeye ni
mwanafunzi, yuko kidato cha pili Mlandizi. Alisema hakuwa na maamuzi ya
kuikataa ndoa hiyo kwani uwezo huo ni wa wazazi wake.Na Global Publisher
Denti
huyo alizidi kuweka wazi kwamba, chanzo kikubwa cha kuozeshwa kwake ni kutokana
na ugumu wa maisha ulioko katika familia hali iliyomsukuma baba yake mzazi
kumshawishi aolewe na kaka yake.
Alisema
kuwa aliambiwa atakapoolewa, mumewe huyo angeendelea kumsomesha jambo ambalo
halikufanyika.
‘’Mimi nilikubali niolewe ili
baadaye nipelekwe shule kwani wazazi wangu hawana pesa za kunisomesha na mimi
siwezi kukataa kwa sababu wazazi ndiyo wameamua,’’ alisema.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa baadhi ya ndugu, dini ya wawili hao inaruhusu kumuoa mtoto
wa mama’ke mkubwa endapo atakuwa amefikisha umri wa miaka 18 haki ambayo kwa
mwanafunzi huyo haipo.
Msemaji
wa dawati la jinsia Wilaya ya Kinondoni, Dar, Inspekta Prisca Komba alisema
kuwa :
‘’Kwa mujibu wa sheria na
taratibu za utamaduni wetu si ruhusa kuoa mtoto wa mama mkubwa tena akiwa bado
mwanafunzi, mimi naona ni kuvunja sheria na ni lazima huyu bwana afunguliwe
jalada la uchunguzi.”
Kaizilege
amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa Kumbukumbu MAG/RB/9015/2013, mara
uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.
via-GPL

0 comments:
Post a Comment