MSHAMBULIAJI WA POLISI MORO SC MESHACK SELEMAN AMBAPO TIMU YAKE IPO KATIKA LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU WA MWAKA 2013/2014.
Timu nne za Morogoro zinashiriki Ligi Kuu na L ligi daraja la Kkwanza Tanzania Bbara msimu huu zipo katika maandalizi makali.
Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Katibu
Mtendaji wa chama cha soka Mmkoa wa Morogoro (MRFA) Hamis Semka alisema
timu za mkoa huo zinazosh
iriki ligi kuu na daraja la kwanza Tanzania bara zipo katika maandalizi ya mwisho.
iriki ligi kuu na daraja la kwanza Tanzania bara zipo katika maandalizi ya mwisho.
Semka alisema kwa sasa Mmkoa wa Morogoro una jumla
ya timu nne ambazo ni Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani, inayoshiriki
ligi kuu, huku Polisi Moro, Burkina Fc na Mkamba Rangers zote zipo ligi daraja la kwanza.
“Msimu wa mwaka 2012/2013 Morogoro tulikuwa na
timu mbili za ligi kuu ikiwemo Mtibwa Sugar na Polisi Moro SC na katika
ligi daraja kwanza nazo zilikuwa mbili za Mkamba Rangers na Burkina FC,
lakini hakuna iliyofanikiwa kupanda daraja na kucheza ligi kuu zaidi ya Polisi Moro SC kushuka daraja.”
Kwa sasa ligi daraja la kwanza kwa msimu wa mwaka
2013/2014 kuna timu tatu baada ya Polisi Moro SC kuongeza idadi katika
ligi hiyo kufuatia kucheza msimu mmoja tangu ipande daraja na kucheza
ligi kuu huku Mtibwa Sugar ikibakiwa na pekee katika ligi kuu.
Semka alisema kuwa katika maandalizi ya mwisho
kabla ya kuingia katika ligi hizo chama cha soka kimeandaa michezo ya
kirafiki kwa timu zote za kujipima nguvu huku Mtibwa Sugar ikicheza
mchezo wake dhidi Prinson katika uwanja wa Jamhuri Morogoro (jana) juzi
katika mchezo uliomalizika kwa sare tasa ya 0-0.
“Leo (jana) timu ya Burkina FC inayoshiriki ligi
daraja la kwanza ilitarajiwa kucheza na Prison, Polisi Moro SC
ikijiwinda na Mbeya City ya Jijini Mbeya iliyopanda ligi kuu msimu huu katika
Uwanja wa jamhuri Morogoro katika mchezo utaopigwa Agosti 13 wakati
Agosti 14 Mkamba Rangers nayo itacheza na Prinson katika Uwanja wa CCM
Mkamba,” alisema Semka.

0 comments:
Post a Comment