DAR ES SALAAM.
SIKU moja baada ya kufanya ziara ya ghafla Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema leo ataweka hadharani majina ya watu wanaosafirisha dawa za kulevya nchini.
SIKU moja baada ya kufanya ziara ya ghafla Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema leo ataweka hadharani majina ya watu wanaosafirisha dawa za kulevya nchini.
Dk Mwakyembe juzi alifanya ziara hiyo JNIA kukagua
utendaji kazi kwenye uwanja huo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea
kashfa ya kupitishwa kwa dawa za kulevya na baadhi ya Watanzania
wakiwamo wasanii kukam
atwa sehemu mbalimbali duniani.
atwa sehemu mbalimbali duniani.
Aidha, hatua ya waziri huyo imekuja siku tatu
baada ya ahadi aliyotoa akiwa Mwanza kwamba katika kipindi cha wiki
mbili kuanzia juzi, atahakikisha anawakamata vigogo wote walio katika
mtandao wa usafirishaji na uingizaji wa dawa za kulevya kupitia viwanja
vyote vya ndege nchini.
Akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa
ya Vijana iliyoandaliwa na Taasisi ya Jitambue Foundation,
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana, Dk Mwakyembe alisema yuko
tayari kufa katika vita hivyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake
jana, Dk Mwakyembe alisema: “Kesho (leo) nitawataja wanaojihusisha na
dawa za kulevya. Kwa sasa nakamilisha ushahidi wa kutosha ikiwa ni
pamoja na picha za wahusika.”
Aliwaonyesha waandishi wa habari picha ya
mtuhumiwa mmoja ambaye alisema alikamatwa saa nane baada ya waziri huyo
kufanya ziara uwanjani hapo. “Ninataka watu wafahamu wanaoliingiza taifa
hili katika aibu hii, ambayo inasababisha Watanzania wasiaminike katika
viwanja vya ndege vya mataifa mengine.”
“Hatuwezi kuwa taifa la kuogopaogopa, hii ni vita
ya kusafisha nchi yetu, kwani ni nani mwenye mkataba na Mungu kuwa
ataishi milele?” alihoji Waziri huyo alipokuwa akijibu swali kuwa suala
la kuwataja watu wanaowafichua wasafirisha unga linaweza likaweka rehani
maisha yake.
“Kama hupendi joto usiingie jikoni”, alisema.
Akizungumzia watendaji wa JNIA kuhusiana na dawa
za kulevya, alisema: “Mfanyakazi yeyote atakayebainika kuhusika
kuwasaidia wasafirisha unga atafukuzwa kazi na ambaye atafanya juhudi ya
kuwakamata wasafirishaji hao atapewa zawadi.”
“Kuna watu wanadhani tunafanya mzaha katika jambo
hili. Jana baada ya mimi kuondoka usiku wa saa 2:30 huyu (kijana
aliyekamatwa) akaingia na mzigo,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza kuwa
alikamatwa na kete 86 za dawa aina ya heroini na misokoto 34 ya bangi
aliyokuwa akiisafirisha kwenda Italia kupitia Zurich.
Aliiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuwatunuku wafanyakazi waliofanikisha kukamatwa kwa kijana huyo.
Akizungumzia hali ya Uwanja wa JNIA baada ya
kufanya ziara juzi, Dk Mwakyembe alisema tatizo halipo kwenye vitendea
kazi, bali wafanyakazi wasiokuwa waaminifu. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment