Wakati msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ukielekea Wilayani Missenyi kukagua sehemu utakapojengwa uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Omukajunguti, gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 570 BYU lilowabeba Waheshimiwa Wabunge 11 lilipata hitilafu na kutaka kuungua.P.T
Ajali hiyo ilitokea eneo la Mwanzo Mgumu kilometa moja kutoka mpakani mwa Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi ambapo gari hilo aina ya costa lilianza kutoa moshi mwingi kwa upande wa nyuma wakati likiwa kwenye mwendo mkali na kuleta hofu kubwa kwa abiria walikuwemo ndani ya gari hilo.Mara baada ya dereva kugundua kuwa gari analoendesha linataka kuungua alilisimamisha na kuwaambia abiria wake kuwa gari linaungua.SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment