MWANASOKA bora wa Afrika na mshambuliaji wa Cameroun Samuel Eto'o amesainisi mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea klabu ya Chelsea huku akipokea mshahara wenye thamani ya Pauni Milioni 7 kwa mwaka.
Eto'o mwenye umri wa miaka 32 ametambulishwa rasmi leo baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Mshambuliaji huyo aliwasili mjini London juzi usiku kwa treni kutoka Ufaransa hadi
Stesheni ya St. Pancras, alisema.
"Nimeona ubora ambao wanao Chelsea, na
nimekuwa nikimfurahia sana Jose Mourinho kabla, hivyo wakati nafasi
inapotokea, huwa nafurahia kuichukua.
Eto'o akionyesha jezi ya Chelsea atakayo itumia katika michezo ya klabu hiyo.
Hapa akisaini mkataba huku akishuhudiwa na Katibu wa Chelsea, David Barnard.
0 comments:
Post a Comment