MADIWANI 8 KUTOKA BUKOBA WALIOIBUKA KIDEDEA
Diwani
wa kata ya Kashai ambaye pia ni mwenyekiti wa wilaya Bukoba mjini
akipongezwa na wananchi muda mfupi baada ya maamuzi ya alimashauri kuu
ya ya mkoa kutenguliwa
Diwani Alexander Ngalina wa Kata Buhembe na Naibu Meya
Diwani Dauda Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo
Diwani Samweli Ruangisa wa kata ya Kitendaguro
Diwani Deusdedith Mutakyawa kata Nyanga
Diwani Yusuf Ngaiza wa kata ya Kashai na mwenyekiti wa CCM Bukoba mjini
Diwani Robert Katunzi wa kata ya Hamugembe
Diwani Murungi Kichwabuta wa viti maalum na mjumbe baraza kuu la Taifa la wanawake
Hongereni sana jamani....
Ni furaha kwa wanachi wa Manispaa ya Bukoba baada ya Nape kutangaza
Murungi akitabasamu
Ni furaha kila pembe
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa Abdul Kagasheki akiwa na wananchi mbalimbali wakifurahia kauli ya Nape
Wanachi wakishangilia kauli ya Nape.
Diwani viti maalumu Murungi Kichwabuta muda mfupi baada ya Nape
kutengua maamuzi ya kufukuzwa kwa madiwani 8 wa ccm akiwa na Diwani wa
kata ya Bakoba Felician Bigambo wa CUF
Diwani
wa kata ya Bakoba (CUF) Feliciani Bigambo akipoongea na wananchi.
Amesema wananchi wangewashangaa CCM kuona watetea haki za wananchi ndio
wanaonekana maadui na kukumbatia mafisadi, na kwamba kama madiwani
wanafanya kazi kwa sheria na kanunu za vikao,hivyo watahakikisha haki za
wananchi zinapatikana
Katibu mwenezi wa CCM Bukoba mjini Kamadhani Kambuka akieleza kuridhishwa kwake na kauli ya Nape kupitia vyombo vya habari
Diwani
wa kata ya Bakoba Felician Bigambo (CUF) akiwaeleza wananchi kuwa Nape
amefanya jambo la msingi kutengua maamuzi ya watu wachache
wanaokumbatia mafisadi na kuwakatisha madiwani tamaa wanaodai haki ya
wananchi wa Bukoba mjini. Amesema madiwani wanafanya kazi kwa taratibu
na sheria na kanuni, hivyo watahakikisha haki inapatikana kwa
kushirikiana na madiwani wa CCM wanaojari kero na haki za wananchi
waliowachagua na sio kikundi cha watu wachache wanaokumbatia mafisadi
Nape akizungumza na Waandishi leo, Dar es Salaam |
HATIMA
ya madiwani wanane wa CCM katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba,
waliovuliwa uongozi na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa Kagera, sasa ipo
mikononi mwa kamati Kuu ya CCM.
Hatima
hiyo, imetangazwa leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata
hilo.
Akizungumza
na waandishi, Nape amesema kwamba licha ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa
wa Kagera kutangaza uamuzi wake wa kuwafutia madiwani hao dhamana ya
CCM, jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku moja
kilichofanyika mjini Bukoba, CCM Makao Mkuu imewataka madiwani hao
kuendelea na kazi kama kawaida wakati wakisubiri maamuzi ya Kamati Kuu
ya CCM ambayo itakutana mjini Dodoma Agosti 23, mwaka huu.
"Kwa
mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye
vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya
Mkoa sio wa mwisho. Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe", alisema Nape na kuongeza;
"Hivyo
basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa
kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini
Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa
Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera".
Nape
alisema, pia CCM makao makuu wamepokea barua ya madiwani hao kukata
rufa kupinga uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa msingi wa madai
ya kukiukwa kwa utaratibu katika kufikia uamuzi huo.
Alisema,
wakati sakata hilo likiwa bado lipo katika hali hiyo, CCM inawasihi
wananchi wa Bukoba na Kata husika, wanachama na viongozi wote kuwa
watulivu katika kipindi hiki ambapo suala hili linashughulikiwa na vikao
vya Kitaifa.
Akifafanua
zaidi Nape amekanusha kwamba, Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete
alipokuwa katika ziara ya kiserikali mkoani Kagera, alitumia fursa hiyo
pia kuwapatanisha madiwani na Meya katika mgogoro unaodaiwa kuota mizizi
baina yao.
Nape
amesema, Rais Kikwete aliagiza hatua za kumaliza mgogoro huo zimalizwe
kwa kufuata sheria na kanuni kwa lengo la kuhakikisha kuwa hakuna upande
utakaoonewa au akupendelewa.
Akitangaza
jana Katibu wa CCM wa mkoa wa Kagera, Avelin Mushi,aliwataja madiwani
waliotimuliwa kuwa ni, Yusuph Ngaiza (Kata Kashai) ambaye pia ni
Mwenyekiti wa CCM wilaya Bukoba, Samwel Ruangisa (Kitendagulo) ambaye ni
Meya mstaafu na Mkuu wa mkoa wa mkoa wa kwanza wa mkoa wa Kagera,
Murungi Kichwabuta (Viti maalumu) Deusdedith Mutakyawa (Nyanga) Richard
Gaspal (Miembeni)Alexander Ngalinda (Buhembe) ambaye pia alikuwa Naibu
MeyaDauda Kalumuna (Ijuganyondo) na Robert Katunzi wa kata Hamugembe.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment