VIONGOZI waandamizi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Taifa akiwemo mwenyekiti wao Bw Freema Mbowe, Mbunge wa Singida Mashariki ambae ni Mnadhimu
Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu na mwenyeji wao mbunge wa
jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wakamatwa na polisi mkoani
Iringa Viongozi hao wamekam
atwa leo majira ya saa 3 asubuhi kati kati ya mji wa Iringa wakati wakitokea eneo la Kihesa kuelekea Bungeni mjini Dodoma kwa shughuli za kibunge kabla ya jeshi la polisi kuwatia matatani na kuwafikisha kituo cha polisi.
atwa leo majira ya saa 3 asubuhi kati kati ya mji wa Iringa wakati wakitokea eneo la Kihesa kuelekea Bungeni mjini Dodoma kwa shughuli za kibunge kabla ya jeshi la polisi kuwatia matatani na kuwafikisha kituo cha polisi.
Akithibitisha
kukamatwa viongozi hao kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan
Mungi alisema kuwa viongozi hao walikamatwa kwa mahojiano kutokana na
kutoa kauli hatarishi kwa amani wakati wa mkutano wao uliofanyika katika
uwanja wa Mwembetogwa kwa ajili ya mabaraza ya ukusanyaji wa maoni ni
rasmu ya katiba.
Kamanda
Mungi alisema kuwa kibali ambacho Chadema walipewa kilikuwa kikianza saa
9 Alasili hadi saa 12 .;00 ila wao waliendelea na mkutano huo hadi
majira ya saa 12 .25 na kila walipofuatwa zaidi ya mara moja kuelezwa
kuhusu muda wa kibali chao kuisha bado viongozi hao waliendelea
kuendesha mkutano huo huku wakitumia vipasa sauti kutoa maneno ya
dhahaka dhidi ya jeshi la polisi.
Hata
hivyo alisema kuwa jeshi la polisi lilishindwa kutumia nguvu kwa
kuwakamata ama kuwashusha viongozi hao jukwaani wakati wa mkutano huo
kama njia ya kuepusha vurugu ambazo zingeweza kutokea iwapo nguvu
zingetumika kuwashusha kwa kuvunja sheria za nchi .Chanzo Matukio Daima.
"Tunawashikilia
viongozi hao kutokana na kutoa kauli hatarishi wakati wa mkutano wao wa
jana (juzi) uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa ....kwani kibali chao
kilikuwa kikiisha saa 12 .00 jioni ila wao walizidisha muda na maofisi
wa polisi waliokuwepo waliwafuata na kuwakumbusha juu ya muda waliopewa
katika kibali chao ila wao badala ya kusitisha mkutano walitumia kipasa
zauti kujibu na kutoa kauli cha hatarishi ....Jeshi la polisi lilitumia
busara na kuwaacha hadi walipomaliza na asubuhi tuliwakamata kitaalam
bila ya kutokea vurugu zozote"
Alisema kuwa viongozi hao hadi majira ya saa 5 leo asubuhi walikuwa
wakiendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na kuwa kufikishwa ama
kutofikishwa mahakamani kutajulikana mara baada ya mahojiano hayo .
Mwenyekiti
wa Chadema wilaya ya Iringa Suzana Mgonakulima alisema kuwa jumla ya
waliokamatwa jana ni viongozi wanne akiwemo Mbowe, mbunge Msigwa , Lissu
pamoja na diwani wa kata ya Mvinjeni katika Manispaa ya Iringa Frank
Nyalusi .
Mngonakulima
alilitaka jeshi la polisi kutimiza wajibu wake bila kutumiwa na chama
chochote cha siasa ama mtu yeyote katika shughuli zao kwani kwa kufanya
hivyo ni kuondoa imani ya polisi na wananchi.
Kuhusiana
na kumamatwa na kuachiwa kwa viongozi hoa alisema kuwa viongozi hao
waliachiwa majira ya saa 5.30 asubuhi baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya
masaa matatu ambapo kila mmoja alitakiwa kuthaminiwa na mtu mmoja kwa
dhamana ya Tsh milioni 2 na wote walikidhi masharti ya dhamana na
kuruhusiwa kuendelea na safari hadi hapo watakapotakiwa kufika polisi .
"
Tunawashangaa sana polisi Iringa Chadema kuzidisha muda dakika 5 imekuwa
tatizo mbona CCM wamekuwa wakifanya mikutano yao hadi saa 1 usiku bila
viongozi wake kukamatwa ....Chadema hatuna tatizo kwa kuonewa na huu si
mkutano wa kampeni ni mkutano wa kukusanya maoni ya katiba ambao
hatutapewa muda kamili na tume ...ila tunawasamehe bure polisi"alisema
mwenekiti huyo wa Chadema Iringa mjini.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment