WANARIADHA Rose Seif na Tumain Elisha jana waliuongoza Mkoa wa Pwani kutwaa medali za dhahabu kwenye fainali ya kuruka chini mruko mmoja (long jump) na kuruka chini miruko mitatu (tripple jump) kwenye mashindano ya riadha ya taifa yaliyomalizika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Tumain ndiye alikuwa wa kwanza kutwaa dhahabu
kwenye fainali ya long jump akiruka umbali wa mita 4 na cm 64.Ushindi wa
Pwani uliendekezwa na Rose Seif kwen
ye fainali ya tripple jump akiruka umbali wa mita 10 na cm 16.
ye fainali ya tripple jump akiruka umbali wa mita 10 na cm 16.
Medali ya pili kwenye tripple jump ilichukuliwa na
Tumain aliyeruka mita 10 na cm 00 na Rose akichukua medali kama hiyo
kwenye long jump akiruka mita 4 na cm 54.
Nafasi ya tatu kwenye tripple Jump ilichukuliwa na Suzan Msoka wa Mwanza aliyeruka umbali wa mita 9 na cm 93.
Kwenye tripple jump upande wa wavulana, Michael
Gwandu wa Manyara aliibuka kinara akiruka umbali wa mita 13 na cm 09,
huku Micheal Danford wa Kilimanjaro akikamata nafasi ya pili akiruka
mita 13 na cm 29 na Denis David wa Kagera akichukua medali ya tatu ya
Shaba akiruka umbali wa mita 13:19.
Kwenye fainali ya mita 10,000 ya wavulana, Ezekiel
Jafari wa Kagera akiibuka kinara akitumia dakika 30:07:37, huku Joseph
Theophil wa Arusha akikamata nafasi ya pili (30:08:70) na Paulo Itambu
wa Singida akikamata nafasi ya tatu (30:13:90).
Mita 5000, Alphonce Felix wa Kagera alikuwa wa
kwanza kwa kutumia dakika 14:35:15, huku Joseph Theophil wa Arusha
akitwaa medali ya Fedha (14:34:50) na Nyangero Patrick wa Kagera akikamata nafasi ya tatu (14:43:59).
Mita 400, Rose Seif wa Pwani aliibuka kinara
(1:03:20), huku Filomena Magine wa Mwanza akikamata nafasi ya pili
(1:04:87) na nafasi ya tatu, Yedida Paulo wa Shinyanga (1:06:42).
Mita 100, Laurent Masatu wa Arusha aliibuka kinara
akitumia sekunde 10:82, Taratibu Machaku wa Tanga nafasi ya pili
sekunde 11:01 na Adinan Haruna wa Kilimanjaro sekunde 11:03.
Katika fainali ya mita 400, Rose Seif wa Pwani
aliibuka kinara akitumia dakika 1:03:20, Filomena Magine wa Mwanza
akitwaa medali ya fedha dakika 1:04:87 na Yedida Paulo wa Shinyanga
akikamata nafasi ya tatu dakika 1:06:42.
0 comments:
Post a Comment