BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HII NDIYO TASWIRA YA MASHINDANO YA TAIFA YA RIADHA MOROGORO 2013 SIKU YA KWANZA.

Mwanariadha akiajiandaa kukimbia mbio fupi za mita 100 uwanja wa jamhuri Morogoro. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
 
 Wasichana wakitimua mbio za mita 100 katika mash
indano hayo.
PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
 Wanaume mita 400.
Mita 400.
 
 Mita 800.
 Mita 100
 Mita 100 kupokezana vijiti wasichana.
Mita 100 wavulana mchujo.
Morogoro. 
Mashindano ya Riadha ya Taifa, yameanza kutimua vumbi leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa huku zaidi ya wanariadha 450 wakitarajiwa kuchuana kuwania medali.
Tayari wanariadha kutoka mikoa mbalimbali wameshawasili mjini hapa.
Mashindano hayo yamekuwa alama ya maandalizi kwa ajili ya kusaka vipaji vya kushiriki mashindano ya kimataifa, kama Jumuiya ya Madola mwakani, na yale ya Afrika ya vijana mwaka huu nchini Maurtius.
Makocha wa timu shiriki walitambiana, huku kila mmoja akijinadi kutwaa medali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti muda mfupi baada ya kuwasili mjini Morogoro, makocha hao kila mmoja alidai timu yake kutwaa ubingwa.
“Vijana wako fiti na bahati nzuri tuna wanariadha wa michezo ya miruko, mitupo na mbio. Natoa tahadhari kwa mikoa mingine wajiandae kupokea vichapo,” alitamba kocha wa Pwani, Robert Kalyahe.
Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Dar es Salaam, Zainabu Mbiro alisema kuwa mkoa wake umejipanga vizuri kutwaa medali kibao kwenye mashindano hayo.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka alisema maandalizi yote yamekamilika na mbio zitaanza saa 2:30 asubuhi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: