BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JK HII NI AIBU KWA TAIFA: MHADHIRI UDSM AUAWA KINYAMA DAR, ZANZIBAR RAIA WA UINGEREZA WAONGEZA IDADI YA WATU WALIOMWAGIWA TINDIKALI,

Kate Gee (18) na Kirstie Trup (18)Patrick Rweyongeza (32).

DAR ES SALAAM/ZANZIBAR.
MAUAJI, mashambulizi ya kudhuru mwili na uporaji vimeendelea kuchafua taswira ya Tanzania baada ya juzi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuuawa kwa kupigwa risasi na watu ambao hawajafahamika, raia wawili wa Uingereza kumwagiwa tindikali na mfanyabiashara kuporwa zaidi ya Sh40 milioni.

Jana, Rais Jakaya Kikwete alikwenda Hospitali ya Aga Khan kuwajulia hali raia hao wawili wa Uingereza waliomwagiwa tindikali huko Zanzibar, Kate Gee (18) na Kirstie Trup (18) akisema tukio hilo limetia aibu kwa mataifa ya nje na kuliam
uru Jeshi la Polisi kuhakikisha linawakamata na kuwafungulia mashtaka wote waliohusika.

MAUAJI.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura alisema jana kuwa mauaji ya Mhadhiri huyo Msaidizi katika Idara ya Uhandisi na Teknolojia, Patrick Rweyongeza (32) yalitokea juzi saa saba mchana maeneo ya Magomeni Tanesco, Dar es Salaam, wakati marehemu alipokuwa ndani ya gari lake akielekea katikati ya jiji.

“Alipofika maeneo hayo alivamiwa na watu waliokuwa kwenye pikipiki aina ya Boxer ambao walimpiga risasi ya kifua upande wa kulia kisha kutokomea.”

“Baada ya kupigwa risasi alipelekwa Muhimbili lakini kabla ya kuanza kupatiwa matibabu alifariki dunia,” alisema Kamanda Wambura.

Alisema hakuna mtu yoyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo. “...Tunaendelea na upelelezi kufahamu tukio hilo lililofanywa na watu hao kama ni la ujambazi au kisasi.”

Akizungumza nyumbani kwa mjomba wa marehemu Mbweni, Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Uhandisi, Dk John Mahunza alisema Rweyongeza alikutwa na mkasa huo baada ya kutoka benki kuchukua fedha kwa ajili ya shughuli za ofisi.

“Baada ya kuchukua fedha hizo Ubungo, alipanda gari kuelekea Magomeni na kufika maeneo ya Tanesco, walimzingira na kumlazimisha kufungua mlango, lakini aligoma na wakampiga risasi,” alisema.

“Baada ya kumpiga risasi mkononi, walimpora bahasha iliyokuwa na fedha... nadhani wale walikuwa wanamfuatilia tangu alipokuwa benki hadi anatoka. MWANANCHI.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: