RIPOTI
ya Wiki imegundua kuwa, fedha ni hatari kwa afya ya binadamu kwani huweza
kusababisha madhara makubwa.
Katika
uchunguzi, ilibainika kuwa fedha za noti na zile za sarafu huweza kukusanya na
kusamb
aza vimelea vya magonjwa hatari kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa
mwingine.
Kuhakikisha ukweli wa jambo hilo, Ripoti ya Wiki ilifanya mahojiano na
mtaalam wa magonjwa mbalimbali, Dk. Richard Marise na kusema kuwa tafiti
mbalimbali duniani zimeripoti kuhusu vimelea vinavyoweza kusafirishwa kupitia
fedha ambavyo ni Staphylococcus Aureus, Escherichiacoli,Fecal Bacteria na sumu
nyingine.
“Tafiti
nyingi zilizofanywa katika nchi zilizoendelea, zimegundua kuwa vimelea
hatarishi kwenye fedha hasa za noti ambapo vingi hutokana na uchafu utokao kwa
mwanadamu mwenyewe kwa mfano; kinyesi, mkojo na jasho.
“Vimelea
hivyo kwa pamoja husababisha magonjwa kama boils (magonjwa ya ngozi) pneumonia,
toxic shock syndrome (homa za sumu mwilini), diarrhea (kuharisha), gum diseases
(magonjwa ya fizi), homa za vipindi na meningitis (uvumbi wa bongo) ambao kama
hakuna matibabu huweza kusababisha kifo,” alisema Dk. Richard.
Akifafanua
jinsi fedha zinavyoweza kusafirisha magonjwa, daktari huyo alisema fedha huweza
kushikwa na mtu asiyeosha mikono yake kwa maji safi na sabuni baada ya kutoka
kujisaidia, kisha hela hiyo huweza kutua mikononi mwa mtu mwingine ambaye
huacha jasho lake na kuongeza vimelea vya magonjwa mengine juu yake.
Mzunguko
huo unaweza ukawa mkubwa kufikia hatua ya vimelea kusambaa kwa mamilioni ya
watu hivyo kuifanya jamii kuwa katika hatari zaidi ya maambukizi ya ugonjwa
husika.
Dk.
Richard alikazia kuwa, maambukizi hutokea kama mtu aliyeshika hela hizo atagusa
sehemu zenye unyevunyevu kwenye mwili wake kwa mfano jicho, mdomo na pua ambapo
vimelea hivyo vitapata nafasi ya kuingia ndani ya mwili.
Katika
mazingira ya kawaida, fedha zenyewe huhifadhiwa katika mazingira hatarishi
ambapo kuna mifano ya watu kuhifadhi fedha ndani ya nguo za ndani au kwenye
matiti (akina mama zaidi).
Fedha
pia huweza kudondoka kwenye uchafu wa aina mbalimbali na kuokotwa kisha
ikatumika tena.
Imeelezwa
kuwa, ukiachilia mbali kubeba vimelea vya magonjwa, fedha zinaweza kubeba sumu
na madawa ya kulevya juu yake ikiwa itapitia kwenye mikono ya mtu aliyeshika
vitu hivyo.
“Ni
vyema ukatumia fedha kwa uangalifu, usiweke hela mdomoni na ukumbuke
kuosha mikono yako kila mara kwa maji na sabuni ili kujikinga na maambukizi,”
alitahadharisha Dk. Richard.

0 comments:
Post a Comment