BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KERRY AITAKA SYRIA KURUHUSU UCHUNGUZI, NI BAADA YA WATU 355 KUFARIKI DUNIA KUTOKANA NA DALILI ZA SUMU.

Activists wearing gas masks bag a dead cat as they collect samples to check for chemical weapon use, in the Zamalka area, where activists say chemical weapons were used by forces loyal to President Bashar Al-Assad in the eastern suburbs of Damascus August 22, 2013. REUTERS/Bassam Khabieh (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST CONFLICT ANIMALS TPX IMAGES OF THE DAY)
WAZIRI wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amezungumza na waziri mwenzake wa Syria Walid al-Moualem Alhamisi wiki hii na kumweleza kuwa serikali yake inapaswa kuruhusu wakaguzi wa silaha wa Umoja wamataifa. 

Wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa wanatakiwa kuingia katika maeneo yanayodaiwa kuwa shambulio la gesi ya sumu limefanyika.

Kerry amepiga simu "kuweka wazi kuwa iwapo, kama inavyodaiwa, serikali ya Syria haina cha kuficha, inapaswa kuwaruhusu wakaguzi mara moja na wapewe ruhusa bila ya vipingamizi katika maeneo hayo bad
ala ya kuendelea kuyashambulia maeneo yaliyoathirika na kuzuwia kuingia kwa wakaguzi pamoja na kuharibu ushahidi" wizara ya mambo ya kigeni imesema.
A survivor from what activists say is a gas attack rests inside a mosque in the Duma neighbourhood of Damascus August 21, 2013. Syrian activists accused President Bashar al-Assad's forces of launching a gas attack that killed more than 200 people on Wednesday, in what would, if confirmed, be by far the worst reported use of chemical arms in the two-year-old civil war. Syrian state television denied government forces had used poison gas and said the accusations were intended to distract a team of United Nations chemical weapons experts which arrived three days ago. REUTERS/Bassam Khabieh (SYRIA - Tags: CONFLICT POLITICS CIVIL UNREST)
Mtu aliyenusurika akijipumzisha baada ya kupatiwa matibabu.
 
Uhakikisho
"Waziri Kerry amesisitiza zaidi kwamba amepokea uhakikisho kamili kutoka kwa makamanda wa jeshi la Syria kuwa watahakikisha kuingia kwa salama wakaguzi wa umoja wa Mataifa katika maeneo hayo," amesema afisa wa wizara hiyo.

Kerry ambaye alishiriki akiwa hayupo katika Ikulu ya Marekani ya White House katika mkutano kuhusiana na uwezekano wa Marekani kuchukua hatua dhidi ya kile kinachodaiwa kuwa ni matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria, amefanya mawasiliano kadha na wanadiplomasia kadha jana Jumamosi na mawaziri wenzake nchini Saudi Arabia, Jordan na Uturuki, afisa huyo amesema.

Katika mazungumzo yote hayo kwa njia ya simu , waziri Kerry amesisitiza umuhimu wa utambuzi wa haraka wa ukweli na kueleza umihumu na athari za matumizi ya silaha za kemikali, ameongeza afisa huyo.
U.S. Secretary of State John Kerry speaks during the London 11 countries Friends of Syria meeting in Doha June 22, 2013. Western and Arab opponents of Bashar al-Assad met in Qatar on Saturday to tighten coordination of their stepped up support for rebels battling to overthrow the Syrian president. REUTERS/Mohammed Dabbous (QATAR - Tags: POLITICS CONFLICT) Waziri John Kerry wa Marekani.
 
Marekani na Uingereza zajadiliana
Rais wa Marekani pamoja na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron wamekaribia jana Jumamosi kuweka lawama za shambulio hilo la gesi ya sumu karibu na mji mkuu Damascus mikononi mwa majeshi ya rais Bashar al-Assad.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu katika mtaa wa Downing imesema kuwa viongozi wa Marekani na Uingereza , wana wasi wasi mkubwa , kuhusiana na ishara zinazoongezeka kuwa hilo lilikuwa shambulio la silaha za kemikali lililofanywa na utawala wa Syria dhidi ya watu wake.
U.S. President Barack Obama speaks about the economy during a visit to Knox College in Galesburg, Illinois July 24, 2013. REUTERS/Kevin Lamarque (UNITED STATES - Tags: POLITICS BUSINESS) Rais Barack Obam.
 
"Ukweli kwamba rais Assad ameshindwa kutoa ushirikiano na Umoja wa Mataifa kunaashiria kuwa utawala huo una kitu cha kuficha," taarifa hiyo imeongeza, na kudokeza kuwa " matumizi ya silaha la kemikali yatasababisha kuchukuliwa hatua kali kutoka jumuiya ya kimataifa."

Serikali ya Syria pamoja na mahasimu wake wakati huo huo wametupiana lawama kwa matumizi hayo ya silaha za sumu, wakati shirika la kutoa misaada la madaktari wasio na mipaka limesema kiasi ya watu 355 wamefariki kutokana na dalili za "sumu inayoathiri mapafu" kutokana na shambulio la Jumatano, huku maelfu zaidi wakipatiwa matibabu hospitalini.

Iwapo itathibitishwa , shambulio hilo litakuwa baya kabisa la matumizi ya gesi ya sumu tangu Saddam Hussein kutumia gesi ya sumu dhidi ya wanajeshi wa Iran na maeneo ya waasi wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq katika miaka ya 1980.
Angela Kane - Untergeneralsekretärin der Vereinten Nationen für Abrüstungsangelegenheiten. (Foto: dapd/Gemunu Amarasinghe) // Eingestellt von wa Afisa wa Umoja wa Mataifa wa kupunguza silaha Angela Kane.
 
Huenda mambo yameiva
Mazungumzo ya Obama na washauri wake wa masuala ya usalama yamekuja siku moja baada ya waziri wa ulinzi Chuck Hagel kusema wizara yake imewasilisha mapendekezo kadha kwa rais na ameeleza kuwa majeshi ya Marekani yanasogezwa karibu kwa uwezekano wowote wa uamuzi wa kuchukua hatua dhidi ya utawala wa Syria.

Wakati huo huo mkuu wa idara ya kupunguza silaha duniani wa Umoja wa Mataifa , Angela Kane, amewasili mjini Damascus siku ya Jumamosi ( 24.08.2013) kutoa msukumo kwa serikali ya Syria kuwaruhusu wataalamu wa Umoja huo kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za sumu. DW
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: