BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIFO CHA TAJIRI ERASTO MSUYA ALIYEPIGWA RISASI 12 MWILINI NA BUNDIKI YA VITA, WAFANYABIASHARA WA MADINI YA TANZANITE WAHUSISHWA KUPANGA MAUAJI YAKE.

Mwili wa Erasto Msuya (kulia) baada ya kupigwa risasi. Kushoto ni gari alilokuwa anatumia. 
Wanausalama wakiubeba mwili wa marehemu Msuya.

MOSHI/ARUSHA
JESHI la Polisi nchini limesema mauaji ya mfanyabiashara tajiri wa madini wa Mirerani, Erasto Msuya yalipangwa na baadhi ya wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite kwa lengo la kulipiza kisasi.
Kauli hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz ambaye pia alimtaja mfanyabiashara tajiri wa madini kuwa ni miongoni mwa watu waliokam
atwa hadi sasa.
Mfanyabiashara huyo aliuawa kwa kupigwa risasi nyingi kwa bunduki ya kivita aina ya Sub Machine Gun (SMG) Agosti 7 mwaka huu eneo la Mijohoroni wilayani Hai Kilimanjaro, ambapo katika eneo la mauaji hayo lilipo hatua zipatazo 70 kutoka barabara kuu ya Moshi-Arusha, yaliokotwa maganda 21 ya risasi za SMG lakini inaelezwa risasi zilizompata zilikuwa ni 12.
Wakati polisi wakimshikilia mtu anayedaiwa kuhusika na tukio hilo, watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia nyumbani kwa bilionea mwingine Arusha kupora kiasi kikubwa cha pesa kabla ya kumfyatulia risasi mlinzi na kusababisha kifo chake.
Kamanda Boaz aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni pamoja na mfanyabiashara Shariff Mohamed Athman (31) Mkazi wa Kimandolu na dereva aitwaye Mussa Mango (30) Mkazi wa Shangarai Arusha.
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, mwingine aliyekamatwa ni Shwaibu Jumanne Said(38) maarufu kwa jina la Mredii, Mkazi wa Mererani Wilaya ya Simanjiro katika Mkoa wa Manyara.Kamanda Boaz alikataa kueleza ushiriki wao akisema hilo lingeweza kuathiri uchunguzi unaoendelea wa mauaji hayo yaliyotikisa miji ya Arusha, Mererani na Moshi. CHANZO MWANANCHI




Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: