USICHOKIJUA KUHUSU SALIM KIKEKE WA BBC SWAHILI...

PENYE nia pana njia na mtafutaji makini huwa hachoki, ndivyo anavyosema mtaalamu wa masuala ya uchumi, Dk Wayne Dyer wa Marekani katika kitabu chake cha ufanye nini kupata unachokiazimia.
Licha ya kauli hii ya Dk Dyneer, kuna
vijana wengi nchini wanaonekana wamekata tamaa; Wengine hufikiri kwamba
kama umezaliwa katika familia duni, maana yake utakuwa na maisha duni
milele, huku wale ambao wamezaliwa katika familia tajiri, wanafikiri
wataendelea kuwa tajiri.
Hata hivyo ukweli ni kwamba mtu yeyote
anaweza kuwa na maisha bora, kama anavyosema msomi Hope Clark katika
kitabu chake Fedha za Waandishi cha hivi karibuni nchini Ireland, kwamba
siri ya kufanikiwa katika maisha ni kuishi kwa malengo, kuishi vizuri
na watu na kupenda kuwa karibu na wasiokata tamaa.
Mwalimu Julius Nyerere wakati fulani
amewahi kunukuliwa akisema ‘Uchumi mnao, mmeukalia’.
Kila mtu
alitafsiri alivyoweza, lakini ukweli hasa ni kwamba mtu yeyote
akijipanga vizuri kwa maana ya kutuliza akili yake, kukaa na watu wa
kumshauri vizuri na kufanyia kazi mambo au mipango anayoipanga, anaweza
kufanikiwa anachotaka...Ni ukweli kuwa kuna wengi wana maisha duni kwa
sababu pamoja na mambo mengine ya tabia zao za kukata tamaa, waoga wa
kuthubutu.
Wengi wanasubiri wengine, wanalalamikia wengine zaidi
Mwalimu alisisitiza, nitamnukuu;
“Hatuwezi kusubiri hadi watoto wetu walio shuleni wamalize elimu yao
ndipo tupate maendeleo ya kiuchumi na kijamii.”
Kwa hali yoyote ambayo mtu inamsumbua
katika maisha yake ni vizuri kuangalia namna ya kujitegemea, badala ya
kulalamikia wengine, anasema mshauri maarufu Marekani, David Kudler
katika chapisho lake alilolipa jina Namna ya Kufanikiwa katika maisha.
Huu ndiyo ukweli wenyewe
Vijana wengi hapa nchini wamekuwa
wakitamani sana kufikia mafanikio lakini wengi wanalalamikia kuwa
wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa mbinu sahihi za
kuwafikisha kwenye kilele cha mafanikio wanayotaka.
Wachambuzi wa
masuala ya uchumi akiwemo Profesa Muhammad Yunus ambaye anasifika kwa
kuinua maendeleo kwa watu wa hali ya chini Bangladesh, wanasema ili
kufikia mafanikio ni lazima uchukue hatua kwa nafasi uliyonayo, bila
kujali ikoje, hii itakusaidia kupata chachu ya kuongeza kasi ya
kutekeleza hatua moja baada ya nyingine katika safari yako.
Kuna wengi wamekuwa wakiwaza makubwa,
lakini wanaishia kuona tu wengine wakipaa. Hata hivyo ni wazi kwamba
ushindi huja baada ya kufanya harakati za kuutaka huo ushindi, siyo
kukaa tu na kulalamika kama wafanyavyo baadhi ya watu.
Kati ya vijana ambao wanaonekana
kupambana hadi kuweza kujenga majina na heshima zao Duniani ni Salim
Kikeke; Ni mtu ambaye kama angekata tamaa hakika asingefika aliko sasa.
Sasa amekuwa ni mtu wa kujadiliwa na
umaarufu wake hauko tu Tanzania, bali maeneo mengi ya Dunia hasa
kunakozungumzwa Kiswahili. Huyu mtu ni kati ya watangazaji wakongwe na
kivutio cha watu wengi kutoka barani Afrika na duniani kote, lakini
katokea wapi?

amewahi kunukuliwa akisema ‘Uchumi mnao, mmeukalia’. Kila mtu

0 comments:
Post a Comment