FRANCIS CHEKA (SMG).
Chiotcha Chimwemwe.
Cheka aliyasema hayo jana katika mahojiano na
gazeti hili mara baada ya zoezi la kupima uzito na afya kwenye ukumbi wa
Hoteli ya Blue Room mjini hapa.
“Ni lazima nishinde ili kulinda heshima yangu, najua litakuwa pambano gumu lakini Chimwemwe hawezi kunipiga,” alisema Cheka.
Jioni hii Cheka na Chimwemwe wanam
aliza ubishi wa nani mkali baina yao kwenye Uwanja wa Jamhuri katika pambano la uzani wa ‘Super Middle’ raundi nane.
aliza ubishi wa nani mkali baina yao kwenye Uwanja wa Jamhuri katika pambano la uzani wa ‘Super Middle’ raundi nane.
Katika zoezi la kupima uzito, Chimwemwe alikuwa na
kilo 73, huku Cheka akiwa na kilo 75, uzito ambao Chama cha Ngumi za
Kulipwa cha PST kimeeleza hauna tatizo.
Pambano la Cheka limebeba hisia za mashabiki wengi wa bondia huyo, ambapo baadhi wanaamini atashinda.
Pambano la leo litakuwa la pili kuwakutanisha
Cheka na Chimwemwe, ambapo pambano la kwanza Cheka alishinda kwa pointi
za majaji 2-1 mwaka jana jijini Arusha.
Kwa mujibu wa promota wa pambano hilo, Zumo Makame milango ya Uwanja wa Jamhuri itakuwa wazi kuanzia saa nane mchana.
Makame alisema bingwa wa zamani wa dunia wa WBU, Rashid Matumla atazichapa na Maneno Oswald kwenye uzani wa super middle.MWANANCHI

0 comments:
Post a Comment