BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAN UNITED YATAJWA KUINGIA KWENYE VITA YA KUMUWANIA BALE KUFUATIA SKY SPORTS KUTHIBITISHA KUWA SPURS NA MADRID HAKIJAELEWEKA.

Gareth Bale - Tottenham Hotspur midfielder Gareth Bale happy and insists Champions League can return to White Hart LaneMtandao wa Sky Sports umesema vyanzo vyake vya kuaminika vya habari vimeuambia mtandao huo kwamba Tottenham wanafikiria kukubali ofa kutoka kwa klabu kadhaa kwa ajili ya Gareth Bale - na kusisitiza kwamba bado hawajakubaliana na Real Madrid kumuuza winga huyoGareth-Bale-shoots
Real wamekuwa wakiongoza mbio za kumsajili Bale wakati wa dirisha hili la usajili, lakini sasa kumetokea klabu nyingine ambayo inaipa upinzani katika kushinda mbio za kumsaini Bale.

Ripoti nchini Spain wikiendi hii zilikuwa zikisema kwamba Madrid walikuwa wanamalizia taratibu za mwisho za kumsaini Bale katika dili ambalo lingevunja rekodi ya dunia - huku Spurs wakiripotiwa kukubali kumuuza nyota huyo.

Japokuwa, sasa imefahamika hakuna makubaliano yaliyofikiwa baina ya Tottenham na Real na sasa klabu hiyo ya White Hart Lane inafikiria ofa za klabu nyingine.  

Manchester United wamekuwa wakitajwa kuvutiwa na Bale, lakini inabaki kusubiriwa kama David Moyes ndio kocha mwingine aliyejiingiza katika mbio za kumtaka winga huyo mwenye miaka  24.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: