Mtaalam
wa Mitambo wa Radio Imaan na Tv Imaan Muhammad Maembe akimuelekeza
Mwenyekiti wa Islamic Foundation Br Arif Nahadi mitambo inavyofanya kazi
katika jengo jipya la makao makuu ya Radio na Tv Imaan
Hizi ndizo sababu za kufungiwa Radio Imani na Radio Kwa Neema.
KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili
vya radio pamoja na kukipiga faini ya Sh mil 5, kituo cha Clouds FM kutokana na
kukiuka maadili ya utangazaji.
Vituo hivyo viwili vya redio
ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa
miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Morogoro na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani
Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM
kimetakiwa kufuta kipindi chake
cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.
Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM
na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo
ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM
kimetakiwa kutoanzisha kipengele (segment) nyingine inayofanana na Jicho la
Ng'ombe iliyo katika kipindi chao cha asubuhi cha ‘Power breakfast’.
Kituo cha Imani FM kinadaiwa
kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku
kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa uchinjaji wanyama kwa Waislamu na
Wakristu mkoani Geita.
Hata hivyo Kamati ya Maadili
imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu
vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa
kufanya.
Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa
kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro
kwa wananchi ambao wamekuwa wakiviamini
vituo hivyo.
Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma
adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa
habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.
Akizungumza kwa njia ya simu mkurugenzi wa Clouds FM Ruge Mutahaba
alisema haoni tatizo kwa viongozi hao kufikia hatua hiyo kwani wanafanya kazi yao, lakini kwakuwa
wamepewa nafasi ya kukata rufaa watajipanga na kuenda kuwaelewesha maana na
umuhimu wa waliyokuwa wakiyarusha katika sehemu (segment) ya jicho la ngombe
iliyo katika kipindi chao cha asubuhi.
Sababu za kufungiwa:
-Kwa Neema FM Mwanza: Sababu ni
kushabikia maswala ya uchinjaji Mwanza
- Radio Iman FM Morogoro: Kushabikia watu
kutoshiriki Sensa 2012
- Clouds FM: Kushabikia ushoga & kuendesha
kipindi kisichofuata maadili (Jicho la Ng’ombe).
Ambapo kifungo hicho kilianza rasmi Tar 26 feb 2013.
|
0 comments:
Post a Comment