Na Lilian Lucas, Morogoro.
MAONYESHO
ya wakulima nanenane kanda ya mashariki yanaonekana kudorora kutokana na idadi
ndogo ya wananchi wanaohudhuria katika maonyesho hayo na baadhi ya wizara kuwa
na madeni yaliyochangia malengo kutofikiwa.
Mwenyekiti
wa chama cha wakulima kanda ya mashariki TASO Mohamed Mzee akizungumza na
waandishi wa habari katika viwanja vya nanenane alisema kuwa maonyesho ya mwaka
huu yamek
uwa si ya kuridhisha kutokana na kuwapo kwa idadi ndogo watu
wanaojitokeza katika viwanja hivyo.
Aidha
alizitaja wizara za Kilimo,chakula na Ushirika,Viwanda na biashara pamoja na
wizara ya Mifugo na uvuvi zimechangia kwa kiasi kikubwa kutopfikiwa kwa malengo
yaliyokuwa yamewekwa na TASO.
Mzee
alisema wizara hizo zinadaiwa zaidi ya shilingi 56 milioni na kwamba hiyo
imechangia kukwamisha baadhi ya malengo ambayo kamati ilikuwa imejiwekea.
Mwenyekiti
huyo alisema malengo ya TASO kwa mwaka huu ilidhamilia kuweka rami katika
barabara zake ili kupunguza vumbi , kuongeza mabomba ya maji, taa katika
barabara mablimbali sambamba na kumaliza kujenga ukuta katika sehemu ambayo
haina ukuta na kwamba zoezi hilo limekwama kutokana na madeni hayo.
Pia
Mzee alisema hadi sasa TASO inadai kiasi cha shilingi 250 milioni kutoka bodi
mbalimbali, halmashauri pamoja na taasisi huku zikiwa zimebaki siku chache
kumalizika kwa maonyesho hayo na kuongeza kuwa madeni haya yamekuwa sugu.
Alisema
kuwa pamoja na changamoto hizo lakini TASO imejitahidi kuhakikisha maonyesho
hayo yanakuwa na mvuto kwa ikiwa ni kuongeza wateja wapya
wanaonyesha bidhaa zao ili watazamaji waweze kujifunza na kubadilisha
uzoefu.
Mwandishi
waa habari hizi alishuhudia idadi ndogo ya wananchi wanaoingia katika
maonyesho hayo,ambapo baadhi ya wananchi walisema kuwa nanenane ya mwaka huu
haina msisimuko kutokana na uhamasishaji kuwa mdogo.
Wananchi
hao walisema kuwa chanzo kikubwa cha kudorora kwa maonyesho hayo ni kwa miaka
minne mfululizo maonyesho hayo kitaifa yamekuwa yakifanyika kanda ya kati bila
kubadilika.

0 comments:
Post a Comment