
MISRI imetangaza hali ya hatari, Uturuki imelihimiza Baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Jumuiya ya nchi za kiarabu kupata
suluhu ya haraka ya kusimamisha mauaji ya halaiki yanayofanyika nchini
Misri.
amano nchini humo. Hali hiyo ya hatari inatarajiwa kuwepo kwa muda wa mwezi mmoja.
Ghasia Misri
Hali hii imezua ghasia katika miji mingine ya Minya Assiut na Alexandria.
Katika ghasia hizo za leo watu zaidi ya 90 wameuwawawa huku wengine wengi wakipata majeraha mabaya.
Kati ya waliouwawa ni mtoto wa kike wa Mohamed El-Beltagi, kiongozi wa chama cha Udugu wa Kiislamu chake Mohammed Musri na mpiga picha wa shirika la habari la Sky News, Mick Deane, aliye na umri wa miaka 61 aliyeuwawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa kazini.
Viongozi wa Ulaya watoa tamko juu ya Misri
Kutokana na ghasia za leo, viongozi wa Ulaya wamelaani kitendo kilichofanywa na vikosi hivyo dhidi ya kambi za waandamanaji mjini Cairo.
Viongozi hao sasa wametaka kuwepo kwa mazungumzo ya amani haraka iwezekanavyo ili kuirudisha Misri katika hali ya utulivu.
Waziri wa nchi za nje wa Ujerumani Guido Westerwelle
Erdogan amesema jamii hiyo ya Kimataifa sasa hasa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Jumuiya ya nchi za kiarabu zinapaswa kuja na suluhu ya haraka ili kumaliza mauaji yanayofanyika huko.
Miito zaidi ya amani Misri
Hata hivyo Peter Stano msemaji wa Umoja wa Ulaya amesema hawaungi mkono kile kinachoendelea Misri kwa sasa na kwamba wana wasiwasi mkubwa juu ya idadi ya vifo inayoendelea kupanda kutokana na machafuko ya leo.
Naye waziri wa mambo ya nje nchini Ujerumani, Guido Westewelle, amehimiza vyama vyote kuja pamoja ili kufikia maelewano juu ya mustakbali wa Misri.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
Msemaji wa ikulu ya Marekani Josh Earnest, aliyekuwa akiwahutubia vyombo vya habari wakati Rais wa Marekanni Barrack Obama akiwa mapumzikoni kwa siku nane alisema kuwa Misri lazima iheshimu haki za inaadamu ya raia wake.
Wakati huo huo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelaani vikali mauaji nchini Misri na kutaka mazungumzo ya amani yafanyike mara moja. DW.
BOFYA NENO HOME JUU UPANDE WA KULIA ILI KUPATA HABARI NYINGINE NDANI YA BLOG HII.

0 comments:
Post a Comment