BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ETI SHILOLE AMETANDIKWA MAGUMI WAKATI AKITAKA KUMBIA KULIPA DENI !!!!.

Zuwena MohamedMSANII Nyota kwenye tasinia ya muziki na filamu bongo Zuwena Mohamed “ Shilole” mwishoni mwa wiki iliyopita alionja joto ya jiwe baada ya kutiwa mtu kati na akinadada waliokuwa wanamdai kiasi kikubwa cha pesa.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na mmoja wa akinadada hao waliokuwa wanamdai zilisema kuwa wanawake hao waliamua kuchukua hatua za kumtia adabu Shilole baada ya kupata taarifa kuwa siku hiyo alikuwa anahama kwa kukim
bia na teni lao.

 “ Ishu ilikuwa hivi sisi tunamdai huyu dada lakini cha kushangaza amekuwa akitupiga chenga sana na ona alivyokuwa sio mstaarabu kumbe siku hiyo alikuwa anahama na deni letu ndio maana tuliamua kwenda kumzingua” Alisema dada huyo aliomba jina lake lihifadhiwe.
Dada huyo aliendelea kufunguka mengi kuhusu sakata hilo “ Unajua sisi tunafanya biashara zetu hivyo kuna siku Shillole alikuja na kusema amekwama kipesa hivyo tumuazime pesa na tukafanya hivyo lakini cha kushangaza mwezi wa sita huu hataki kurudisha na amekuwa akitukwepa mara kwa mara hivyo majirani ndio wakatushtua kuwa anataka kuhama kwa staili ya kutoroka na deni letu ndipo tulipoenda wanawake wanne na kumshushia kipigo” Alisema dada huyo
Baada ya taarifa hizo Shilole alitafutwa kupita simu yake ya mkononi pamoja na kupita kwenye makoloni yake hakuweza kupatikani isipokuwa majirani mbalimbali walikili kutokea kwa tukio hilo la kufedhehesha kwa msanii huyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: