BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA AWAPOZA WANAHABARI NCHINI.

DAR ES SALAAM. 
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba amesema kabla ya kuundwa kwa Katiba Mpya sheria zote zinazokandamiza uhuru wa habari zitaangaliwa kwa sababu katiba ni sheria mama na sheria yoyote itakayopingana na katiba ni batili.
Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau wa tasnia ya habari kuhusu sheria mbalim
bali ambazo zimekuwa zikikandamiza uhuru wa habari.
Akizungumza jana wakati wa mkutano ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kujadili rasimu ya Katiba Mpya, alisema Katiba ni sheria mama hivyo sheria yoyote itakayopingana na katiba itakuwa ni batili.
Alivitaka vyombo vya habari nchini kusikiliza maoni ya wananchi ili kuepuka kupata katiba ya makundi kwani haitakuwa imemaliza tatizo lililosababisha kuunda Katiba Mpya.
“Nafasi ambayo tasnia ya habari itapata kwenye katiba itasaidia kujenga taifa kwa sababu tasnia hii ni ya pekee inayoweza kujenga taifa endapo itatumiwa vizuri kwa kuwasilisha maoni ya wananchi katika uundaji wa katiba na kutengeneza katiba inayokidhi haja za wananchi na kutetea haki zao na hasa walioko vijijini,” alisema Warioba.
Kuhusu suala la Serikali tatu Mwenyekiti huyo alisema “Tumechambua kwa makini tukaweka Serikali tatu sasa wananchi mtuambie ni sawa au si sawa na kama siyo sawa tufanyeje, hayo ndiyo tunayohitaji,”.
Naye Meneja Programu MCT, Pili Mtambalike alisema wanahabari wamepewa fursa ya kujadili na kutoa maoni yanayohusu uhuru wa vyombo vya habari kwa kuzingatia kanuni elekezi kama uhuru wa vyombo vya habari, na haki ya msingi ya kupokea, kuchakata na kusambaza habari, ni mali ya umma kwa pamoja na mtu mmoja mmoja. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: