NG'OMBE zaidi ya 80 wameuawa kikatili kwa kukatwakatwa na wengine kuchinjwa baada ya mifugo kuingia katika mashamba ya wakulima wa vijiji vya Kisara na Mbogo wilaya Mvomero mkoa wa Morogoro.
ITV imeshuhudia mabaki ya nyama na ngozi za na
ndama wachanga waliondolewa katika matumbo ya ngombe waliochinjwa na
kisha nya
ma kuuzwa katika mabucha huku ng'ombe wengine wakiwa wamekatwa miguu na kushindwa kutembea ambapo wamiliki wa ngombe hizo ambao ni wafugaji wamelalamikia wakulima kuchukua hatua mkononi na kuomba serikali kuchukua hatua.

Nao baadhi ya wakulima wa wilayani Mvomero
walioshuhudia tukio hilo wameonyesha kusikitishwa na tukio hilo huku
wakiitaka serikali kuhakikisha inapanga mipango mizuri ili kunusuru
migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kutenga maeneo maalumu kwa shughuli
za kilimo na ufugaji.
Nae mkuu wa wilaya ya Mvomero Antony Mtaka
akizungumzia tukio hilo amesema serikali ya wilaya imeanza kuchukua
hatua kwa kushirikiana na jeshi la polisi ili waliohusika na tukio hilo
wachukuliwe hatua za kisheria huku akiwataka wafugaji kutulia wasilipize
kisasi. CHANZO ITV
0 comments:
Post a Comment